Somo la 1 *Machi 28–Aprili 3 Kujak waYesu

Somo la 1

Kujak waYesu

*Machi 28?Aprili 3

Sabato Mchana

Somo la Juma Hili: Luka 1:2, 3; 2 Tim. 3:16; Luka 1:5?22; Kum. 18:15; Luka

2:9?12,25?32.

Fungu la Kukariri: "`Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu'"

(Luke 1:37).

Injili ya Luka iliandikwa hasa kwa watu wa Mataifa. Luka mwenyewe alikuwa ni mtu wa Mataifa (imeangaziwa katika muktadha wa Wakolosai 4:10?14), kama alivyokuwa Theoilo, ambaye Injili ilikuwa imeandikwa kwake. Kando na kuwa tabibu, Luka alikuwa pia ni mwana-historia mzuri sana. Kwa kuutoa utangulizi wa Injili, Luka anamuweka Yesu katika historia halisi; yaani, anakiweka kisa katika muktadha wa kihistoria wa wakati wake: Herode alikuwa ni Mfalme wa Uyahudi (Luka 1:5), Augusto aliutawala ufalme wote wa Rumi (Luke 2:1), na kuhani aliyekuwa anaitwa Zekaria alikuwa anahudumu katika zamu yake hekaluni, Yerusamu (Luka 1:5, 9). Katika mlango wa 3, Luka anataja nyakati sita za wakati ule zinazohusu huduma ya Yohana Mbatizaji, aliyemtangulia Yesu. Kwa hivyo, Luka anakiweka kisa cha Yesu katika historia-akiangazia watu halisi wa kihistoria, na wakati halisi-ili pasiwepo wazo lolote la uwongo katika maandishi yake. Sharti wasomaji wake waweze kujua na kushangaa kwamba Yesu ni halisi na ya kuwa, kupitia Kwake Mungu ameivamia historia na "`Mwokozi, ndiye Kristo Bwana'" (Luka 2:11).

*Jifunze somo la juma hili kwa maandalizi ya Sabato ya April 4.

5

Jumapili

Machi 29

"Kukuandikia kwa Taratibu"

Matendo 1:1 inatwambia kuwa, kabla kitabu cha Matendo hakijaandikwa, mwandishi wake alikuwa ameandika "Kitabu kile cha kwanza."Swala hili, na ile kuwa vitabu vyote viliandikwa kwa Theoilo, hutusaidia kufahamu kuwa ni mwamdishi mmoja ndiye aliandika vitabu vyote viwili. Vitabu hivyo viwili vinaweza kuwa kama awamu ya 1 na ya 2 ya "Mwanzo na Historia ya Kanisa la Kikristo." Awamu ya 1 ni maelezo ya maisha na kazi ya Yesu (Injili ya Luka) na awamu ya 2 (Matendo ya Mitume) ni maelezo ya usambazaji wa ujumbe wa Yesu na wa kanisa la awali.

Injili iliandikwaje? Soma Luka 1:2, 3 na 2 Timotheo 3:16.

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

Luka alikuwa anatambua juu ya wengi ambao walikuwa wameandika juu ya matukio ambayo yalikuwa yameutikisa mji wa Yerusalemu na kwingineko-- matukio kuhusu Yesu Kristo. Vyanzo vya kazi hiyo ya uandishi vilijumuisha "mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno" (Luka 1:2)--hiyo ikiwaangazia wanafunzi na wale waliokuwa nyakati za Yesu. Luka mwenyewe alikuwa karibu na mashahidi na wahudumu hawa (kama vile Paulo na viongozi wengine wa kiutume) na inawezekana pia Injili iliyoandikwa na Marko na Mathayo. Bila shaka Luka hakuwa ni shahidi kwa kisa cha Yesu, bali alikuwa ni muongofu wa kuaminika na halisi wa Kristo.

Mathayo aliandikwa kwa Wasomaji wa Kiyahudi, akimuangazia Yesu kama Mwalimu Mkuu, mtimilizaji wa unabii, na Mfalme wa Wayahudi. Mara kwa mara alionyesha jinsi tabiri za unabii wa Agano la Kale zilivyotimilizwa katika Kristo. Marko aliandika kwa wasikilizaji wa Kirumi kuhusu Yesu, mtu wa vitendo. Luka, aliyekuwa ni daktari na mtu wa Mataifa, aliandika kwa Wayunani na watu wa Mataifa kuhusu Yesu wa ulimwengu wote--Mwokozi wa ulimwengu. Luka anasema kuwa, kusudi la kuandika kwake lipo mara mbili: ni kumuandikia "kwa taratibu" na kupeana mafundisho makuu ya enzi mpya. Uhakika wa ukweli ulio katika Yesu, ni moja wapo ya kusudi la Injili yake.

Luka, mwandishi wa Maandiko aliyekuwa amevuviwa, alitumia taarifa nyingine katika maandishi yake. Ni wazi kuwa, matumizi yake ya taarifa hizo zingine hakupingi uvuvio au mamlaka ya kile alichoandika. Ni mafundisho gani twapaswa kuwa nayo sisi kama Waadventista wa Sabato kuhusu jinsi uvuvio ufanyavyo kazi kwa waandishi waliovuviwa?

6

Jumatau

"Jina Lake Utamwita Yohana"

Machi 30

Kwa karibu miaka mia nne kimya cha kiungu cha Malaki kilitanda katika historia ya Israeli.Kwa tangazo la kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji na Yesu, kimya hicho kilikuwa kiko karibu kuvunjwa.

Visa vya kuzaliwa kwa Yohana na Yesu vina mambo mengi yanayoenda sambamba. Vyote viwili ni vya kimiujiza: kuhusu cha Yohana, Elisabeti alikuwa amepitisha umri wa kuzaa; kuhusu cha Yesu, bikira alikuwa azae mtoto. Malaika Gabrieli alitangaza ahadi zote mbili za uzazi. Matangazo yote mawili yalipokelewa kwa mshangao, furaha, na kwa kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu. Watoto wote wawili walikuwa wakue kwa nguvu za rohoni (Luka 1:80, 2:40).

Lakini utume na huduma za watoto hawa wawili wa kimiujiza zilikuwa ni tofauti kabisa.Yohana alikuwa ni awe mtengenezaji wa njia kwa ajili ya Yesu (Luka 1:13?17).Yesu ni "`Mwana wa Mungu'" (aya 35) na mtimilizaji wa tabiri za kimasihi za kiunabii (aya 31?33).

Soma Luka 1:5?22. Ijapokuwa Zakaria anaangaziwa kama aliyekuwa "bila lawama," ukosefu wake wa imani kwa tangazo la malaika kulimletea tatizo. Hili linatusaidiaje kuelewa maana hasa ya kuwa "bila lawama" kwa muumini aliye katika Yesu?

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

"Kuzaliwa kwa mwana wa Zakaria, kama kulivyokuwa kuzaliwa kwa mtoto wa Ibrahimu, na kwa yule wa Mariamu, kulikuwa na fundisho kuu la kiroho, ukweli ambao twajifundisha pole pole sana na ambao twausahau kwa haraka. Sisi wenyewe hatuwezi kutenda lolote lililo jema; na lile tusiloweza kutenda litafanywa kwa uwezo wa Mungu kwa kila nafsi ambayo inaamini na kujitoa. Ni kwa njia ya imani mtoto wa ahadi alipeanwa. Ni kwa njia ya imani maisha ya kiroho yanapatikana, na tunawezeshwa kutenda kazi za haki."--Ellen G. White, The Desire of Ages, p. 98.

Muujiza wa Yohana ulikuwa na kusudi lililo wazi la jinsi Mungu anavyoshughulikia watu Wake. Baada ya miaka 400 ya kutokuwepo kwa tabiri zozote za kiunabii katika historia ya Israeli, Yohana alikivunja kimya hicho cha historia hiyo kwa kuuleta ujumbe wenye nguvu na uliokuwa maalumu. Utume na ujumbe wa Yohana ulikuwa ni "`kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.'" (Luka 1:17). Alikuwa awe mtangulizi wa Masihi, yeye ambaye alikuwa atengeneze njia ya utume wa Yesu.

7

Jumanne

"Jina Lake Utamwita Yesu"

Machi 31

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo hakukuwa tukio la kawaida. Kulikuwa kumewekwa katika kalenda ya umilele ya Mungu na "ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke" (Gal. 4:4).Huu ulikuwa ni utimilizo wa ahadi ya kwanza ambayo Mungu aliiweka baada ya kuingia kwa dhambi katika Edeni (Mwa. 3:15).

Soma jozi zifuatazo za Maandiko. Kila jozi inaelezeaje utimilizo wa kimiujiza wa tabiri za kiunabii wa kuzaliwa kwa Yesu? Hii inatwambia nini kuhusu, ni kwa nini tunahitajika kujifunza kuziamini ahadi zote za Mungu? Kum. 18:15; Mdo. 3:22?24; Isa. 7:14; Mat. 1:22, 23; Mika. 5:2; Luka 2:4?7.

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

Miezi sita baada ya Gabrieli kumtangazia Zakaria juu ya tukio lililokuwa linakuja la kuzaliwa kwa Yohana, alimtangazia Mariamu wa Nazareti muujiza mkuu zaidi: kwambabikira "`utapata mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu'" (Luka 1:31).

Kuzaliwa kwa Yesu na bikira kuko kinyume na asili yote, na hakuwezi kuelezewa kwa njia ya kiasili wala katika falsafa ya kiasili. Hata Mariamu alikuwa na swali hili: "`Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?'" (aya 34). Malaika alimhakikishia kwamba hiyo ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu (aya 35), na ya kuwa "`hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu'" (aya 37). Kujitoa kwa Mariamu kwa haraka na kwa uaminifu kulikuwa kwa ajabu: "`na iwe kwangu kama ulivyosema'" (aya 38). Kila swali na kibinadamu, hata liwe la kiasili au la kiakili, sharti lipeane nafasi kwa jawabu la kiungu. Hata liwe ni la Uumbaji au la Msalaba, la Kufanyika mwili au la Ufufuo, la kuanguka kwa manna au la kuja kwa Roho wakati wa Pentekoste--uungu huhitaji kujisalimisha na kukubali kwa mwanadamu.

Mariamu alipolijibu swali lake kwa kujitoa na kujisalimisha kwa kusudi kuu na la umilele la Mungu, Gabrieli alimhakikishia kwa kumpa jibu jingine kuu: "`Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu'" (aya 35).

Baadhi ya tamaduni za kidunia zinaamini kuwa, hatimaye kila kitu sharti kiwe na maelezo ya kiasili au ya kisayansi. Kwa nini mtazamo huu inyu na wa juu juu unakosa uhalisi wa fahari na ukuu wa Mungu?

8

Jumatano

Hori la Bethlehemu

Aprili 1

Luka anakianza kisa cha hori la Bethlehemu kwa mfumo wa kihistoria. Yusufu na Mariamu wanatoka nyumbani mwao huko Nazareti ili wasairi kwenda kwenye mji wa ukoo wao wa Bethlehemu kutokana na agizo la kuwahesabu watu la Kaisari Augusto Mfalme wa Rumi. Hilo lilifanyika wakati Kirenio alikuwa ni liwali wa Shamu. Maelezo haya ya kihistoria yanawafanya wasomi wa Biblia wapendezwe na kujitoa kwa Luka kwa Roho Mtakatifu, ili kwamba aweze kunukuu maelezo ya kina ya ufanyikaji mwili katika muktadha wa kihistoria.

Angazia umaskini wa Yesu kama ulivyo katika Luke 2:7. Linganisha na "nguo za kitoto," "hori," na kutokuwa na "nafasi katika nyumba ya wageni," na maelezo ya Paulo ya ushushwaji wa hadhi ya Yesu yaliyopo katika Wailipi 2:5?8. Ni njia ya aina gani ambayo Yesu alipita kwa niaba yetu?

______________________________________________________________________

Kisa cha hali ya kimaskini ambayo Bwana wa Mbinguni alikubali kuchukua kinaangazia wageni wa kwanza ambao hori ilipokea: wachungaji. "`Habari njema ya furaha kuu'" (Luka 2: 10) haikuwajia matajiri au wenye nguvu, waandishi au makuhani, watawala au wenye uwezo waliokuwa na mvuto katika nchi, bali iliwajia wanyenyekevu na wachungaji waliodharauliwa. Hebu angalia ukuu na ukawaida wa ujumbe huu: Mwokozi amezaliwa kwa ajili yenu. Katika mji wa Daudi. Ndiye Kristo Bwana, Masihi. Mtamkuta amevikwa nguo za kitoto (hii ni tafsiri ya mwandishi). Zawadi ya thamani kuu ya mbinguni ililetwa ikiwa imefungwa kwa njia ya kawaida mno, kinyume na ifanywavyo kwa zawadi. Lakini zawadi hiyo inaleta utukufu kwa "`Mungu,'" "`na duniani . . . amani,'" "`kwa watu aliowaridhia'" (aya 14).

Kumbukumbu ya Luka ya malaika (Luka 2:9?12) inatupatia mambo matatu muhimu ya thiolojia ya Kikristo. Kwanza, habari njema ya injili ipo kwa "`watu wote.'" Katika Yesu, Wayahudi na watu wa Mataifa wanakuwa ni watu wamoja wa Mungu. Pili, Yesu ni Mwokozi; na hakuna mwingine. Tatu, Yesu ndiye Mwokozi na Bwana. Mada hizi tatu, zinazoonekana kwa uwazi na mapema sana katika Luka, baadaye zilikuja kuwa ni msingi wa mahubiri ya mitume, na hasa kwa Paulo.

Hebu ikiria kile tuaminicho kama Wakristo: Muumbaji wa vyote ambavyo viliumbwa (Yoh. 1:1?3) hakuja tu katika ulimwengu huu ulioanguka kama mwanadamu, bali aliishi maisha magumu ambayo Yesu aliyapitia, na hatimaye kusulubiwa msalabani. Ikiwa kweli tunaamini hilo, kwa nini sharti kila kipengele cha maisha yetu kinapaswa kiweze kujitoa kwa ukweli huu wa ajabu? Ni sehemu gani za maisha yako zinaakisi imani yako katika kisa cha Yesu na ni sehemu gani haziakisi?

9

Alhamisi

Mashahidi wa Mwokozi

Aprili 2

Japo Luka aliwaandikia watu wa Mataifa hasa, alizithamini desturi za Kiyahudi zilizokuwemo katika Agano la Kale. Yeye anaunganisha kisa cha Agano Jipya na Agano la Kale na anapeana taswira nzuri ya Mariamu na Yusufu wakimtahiri mtotoYesu siku ya nane na kumpeleka hekaluni, yote hayo yakiwa ni kulingana na sheria ya Kiyahudi (Luka 2:22?24).

Soma Luka 2:25?32. Zingatia vidokezo vitatu kuhusu thiolojia ya wokovu ambayo Simeoni anaviangizia: wokovu upo kupitia kwa Yesu; wokovu unaandaliwa na Mungu; wokovu upo kwa watu wote--kwa watu wa Mataifa na wa Israeli. Kweli hizi zinahusianaje na ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14:6, 7?

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

______________________________________________________________________

Unabii wa Someoni pia ulitabiri mambo mawili muhimu ya huduma ya Yesu.

Kwanza, Kristo "`amewekwa kwa kuanguka na kuinuka kwa wengi walio katika Israeli'" (Luka 2:34). Ni kweli, Kristo ameleta nuru na wokovu kwa wote, lakini sio bila gharama kwa watakaopokea. Katika maswala kuhusu Kristo, hakuna sehemu ya katikati: ni aidha umkubali au umkatae, na wokovu wa mtu hutegemea uamuzi ambao mtu atauchukua. Kristo anahitaji hali yenye msimamo; ni tuwe ndani Yake au la. Wale walio ndani Yake watakuwa ni sehemu ya ufalme Wake; wale wanaomkataa au kutomjali wataanguka chini na kuangamia bila tumaini. Imani katika Kristo ni jambo ambalo halihitaji mjadala.

Pili, Simioni alimtabiria Mariamu, "`upanga utaingia moyoni mwako'" (Luka 2:35). Bila shaka hiyo ilikuwa inauangazia Msalaba ambao Mariamu ataushuhudia. Mariamu na kizazi chote ambacho kimemfuata wanapaswa kukumbuka kwamba, bila Msalaba, hakuna wokovu. Msalaba ndio kiini cha mpango wote wa wokovu.

Wokovu ni zawadi maana hakuna chochote tuwezacho kufanya ili kuweza kuupata. Pia, waweza kuwa ni wenye gharama mno kwa wale ambao wanauhitaji. Kumfuata Kristo kumekugharimu nini, nani kivipi gharama hiyo, hata iweje, sio ghali?

Ijumaa

Aprili 3

Jifunze Zaidi: "Luka, mwandishi wa Injili iliyo na jina lake, alikuwa ni tabibu

wa kimishenari. Katika Maandiko anaitwa `tabibu mpendwa.' Wakolosai 4:14. Mtume Paulo alisikia juu ya ustadi wake wa utabibu, na akaona kwamba yeye ni mtu ambaye Bwana amempatia kazi maalum. Alimtaka ili wafanye kazi pamoja, na kwa muda fulani Luka aliandamana naye katika safari zake kutoka mahali hapa hadi pengine. Wakati fulani, Paulo alimwacha Luka Filipi, ya Makedonia. Hapo aliendeleza kazi kwa miaka kadha, akihudumu kama tabibu na mwalimu wa injili. Katika kazi yake kama tabibu, alihudumia wagonjwa, na kisha aliomba kuwa uwezo wa uponyaji wa Mungu uweze kuwajilia wote waliokuwa wagonjwa. Kwa hivyo, njia ilifunguka kwa ajili ya ujumbe wa injili. Ufanisi wa Luka kama tabibu ulimpatia yeye fursa nyingi za kumhubiri Kristo miongoni mwa watu wa Mataifa. Ni mpango wa kiungu kwamba tutafanya kazi kama vile wanafunzi walivyofanya."--Ellen G. White, The Ministry of Healing, pp. 140, 141.

Maswali ya Kujadili:

1. Ikiwa Luka alitilia maanani kazi zingine za uandishi zilizokuwa zimechapishwa awali wakati wa uandishi wa kitabu chake cha Injili, tunapaswa tueleweje juu ya uvuvio wa Maandiko (2 Tim. 3:16)? Uvuvio unafanyaje kazi? Tazama Ellen G. White, "Uvuvio wa Waandishi wa Kiunabii," Selected Messages, book 1, pp. 15?23.

2. Kuzaa kwa bikira kulitokana na Mungu, kulidhihirisha muujiza, ukuu, na utume Wake. Ni kweli kwamba hiyo imepita ufahamu wa mwanadamu pia. Lakini swali ni "Kwa hivyo?" Ni mambo gani ya kidunia ambayo yamepita ufahamu wa mwanadamu vile vile? Kama Mungu anaishi kweli, na anaouwezo wa kuumba na kuudumisha ulimwengu, kwa nini kitu kama kuzaa kwa bikira kiwe kimeupita uwezo Wake? Ni wale tu walio na mtazamo inyu wa sheria za asili (hasa wale ambao kwa sasa tunawaelewa) wanaweza kuliondoa wazo la uwezekano wa kuzaa kwa bikira. Kinyume cha hayo, wale ambao mtazamo wao wa mambo unajumuisha ukiaumbile (supernatural) hawana sababu yoyote ya kupinga jambo hilo. Hebu angalia kile ambacho malaika alimwambia Mariamu baada ya kumpatia habari za ajabu: "kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu" (Luka 1:37).

3. Mhojaji (interviewer) wa runinga wa Kimarekani anaripotiwa kuwa alisema kwamba, kama angekuwa na fursa, mtu ambaye angependa sana kumhoji angekuwa ni Yesu, na angeweza kumuuliza swali moja tu: "Je, wewe kweli ulizaliwa na bikira?" Kwa nini swali hilo na jawabu lake ni muhimu mno?

11

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download