Www.kenyaplex.com



KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCILKCPE 2006KISWAHILIPAPERSoma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasiumepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.Kandamiza hakujua thamani ___1___ watoto ___2___ siku moja ___3___ na ulimwengu. Alizoeakuwatumikisha watoto wadogo kwa ___4___ kuwaajiri watu wazima asije akajiumiza kwa kuwalipamishahara mikubwa. Siku moja mwanawe mmoja ambaye ___5___ kuyamudu masomo aliamua kuondokanyumbani bila kuaga. Kandamiza alipogundua kuwa mwanawe ___6___ mjini aluhuzunika mno. MoyoniKandamiza alijua kuwa mtoto huyo ___7___ jinsi yeye alivyowafanya watoto wa wengine.A B C D1. Wa la za ya2. Sasa hadi tangu lau3. Alipofunzwa alikofunzwa aliofunzwa aliyefunzwa4. Kuchelewa kupenda kucheka kupendelea5. Hawezi hakuweza hataweza hajaweza6. Ametoroka ametoroshwa ametorokea ametorosha7. Angetesa angemtesa angewatesa angeteswaTaifa lolote___8___ wananchi wenye afya. Magonjwa ___9___ nchi hasara ___10___ pia huwamzigo mzito kwa mtu binafsi. ___12___ ya magonjwa hutokana na___13___usafi. ___14___huweza kuzuiwa iwapo wananchi wataitikia wito wa kunadhifisha makazi ___15___A B C D8. Huhitaji hahitaji yahitaji lihitaji9. Hailetei haileti hayaleti hayailetei10. Ajabu kamwe tu naam11. Bali mbali na ijapokuwa12. Baina baadhi kati zaidi13. Kutodumisha kutodumu kudumisha kudumu14. Hii hizi hiyo haya15. Lao yao zao waoKutoka swali la 16 mpaka 30 chagua jibu lililosahihi16. “Ki” imetumiwaje katika sentensi: Mwenialipokuja alinipata nikifyekaA. Kuonyesha hali ya mashartiB. Kuonyesha hali ya kukanushaC. Kuonyesha hali ya kuendeleaD. Kuonyesha hali ya udogo17. Ni sentensi ipi sahihi?A. Ndizi lililoletwa ni languB. Miti zilizopandwa zimeotaC. Zulia iliyonunuliwa ni zuriD. Wema unaozungumziwa ni huu18. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili, ni sehemuipi iliyo tofauti na zingine?A. PajaB. KiganjaC. PafuD. Goti19. Polepole, vibaya, alasiri, njiani, niA. VieleziB. VivumishiC. NominoD. Viwakilishi20. Methali inayotoa funzo kuwa: jambolinaloonekana zito kwa mwingine laweza kuwarahisi kwako ni;A. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango waziB. Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufiC. Kila mwamba ngoma ngozi huvutia kwakeD. Ganda la muwa la jana chungu kaonakivuno21. Sentensi “Asingalikwenda kwake asubuhiansingalimkuta” ina maana kuwa;A. Hakuenda kwake asubuhi lakini alimkutaB. Alienda kwake asubuhi lakini hakumkutaC. Alienda kwake asubuhi na akamkutaD. Hakuenda kwake asubuhi wala hakumkuta22. Ni maneno yapi ambayo yote ni viunganishi?A. Ila, ingawa, lakini, maadamuB. Huyu, hao, ovyo, naC. Ila, lakini, vizuri, wimaD. Ingawa, isipokuwa, zuri, safi23. Kivumishi cha sifa kutokana na kitenzi angaa ni:A. AngazaB. AngaziaC. AngavuD. Angalau24. kwa maneno ni:A. Subui naneB. Thumuni sabaC. SubuiD. Thumuni25. Kisawe cha neno barobaro niA. BanatiB. KijanaC. MvulanaD. Shaibu26. Nomino habari iko katika ngeli ya:A. U-ZIB. I-IC. U-ID. I-ZI27. Tano ni kwa chokaa. Kitita ni kwaA. PesaB. FunguoC. NdiziD. Ngozi28. Haya ni maumbo gani?A. Pembe tatu, Mche, DuaraB. Pia, Mcheduara, NusuduaraC. Pia, Mchemramba, McheduaraD. Pembe tatu, Pia, Nusuduara29. Chagua usemi halisi ufaao wa:Bahati alisema kuwa angeenda nyumbanikupumzikaA. “Nimeenda nyumbani kupumzika,” BahatialisemaB. “Niende nyumbani kupumzika,” BahatialisemaC. “Nitaenda nyumbani kupumzika,” BahatialisemaD. “Nilienda nyumbani kupumzika,” Bahatialisema30. Yapange maneno yafuatayo kulingana na jinsiyanavyotokea katika kamusi:(i) Bandika(ii) Beua(iii) Birika(iv) BaidikaA. (i) (iv) (ii) (iii)B. (iv) (ii) (iii) (i)C. (ii) (i) (iii) (iv)D. (iv) (i) (ii) (iii)Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 31 mpaka 40Huko Tujueni aliishi mtu kwa jina Mkazeni. Mkazeni alikuwa maarufu katika kutabiri ndoto. Alijulikanapia kwa kuyadadisi mambo yaliyozuka humo kijijini mwao. Kwake kulifurika watu ambao aliwahudumuabila malipo.Wakati fulani Mkazeni alioteshwa kuwa kulikuwa na magari na matrela ambayo yalikuwayakisimamishwa humo kijijini. Madereva wake walikuwa watu waliojaa wadudu tele mwilini. Madereva haowalikuwa wakiwalaghai vijana kijijini huku wakiwaachia “zawadi” zilizileta “vilio”. Alipowaeleza wanakijijiwakamcheka na kumwambia, “sasa nguvu zako za utabiri zinapotea . utawezaje kufikiria kuwa magari hayoyataleta balaa? Magari hubebea mali!”Ingawa maneno hayo yalisemwa kiutaniutani, yalimchoma maini, akaamua kufyata ulimi na kukaza niayake. Alijitahidi kuihimiza aila yake kuhusu umuhimu wa tabia njema.Siku nyingine tena akaota ndoto kuwa huko Tujueni kumeingia joka kubwa lililowameza vijanawengi.Ingawa wanakijiji walikuwa wamepuuza hapo awali; aliwafafanulia ndoto hiyo nao wakazidikumcheka. “Sasa tena utabiri umeleta mambo ya nyoka? Tangu uzaliwe umewahi kumwona nyoka kamahuyo?” hapo Mkazeni akaona amedharauliwa kupita kiasi, akaamua “kujimezea” utabiri wake mwenyewe,lake liwe jicho tu. Watu ambao waliamua kutojihadhari kabla ya hatari, angewafanya nini? Kidole kimojakingevunjaje chawa?Miaka michache ikapita, nayo magari na matrela ya kikweli yakafika pale na kupafanya kituo chamapumziko. Madereva wakaiona sehemu hiyo ikiwa na starehe nyingi. Tujueni ikajulikana. Bisharamadukani na kwenye masoko zikaongezeka.Baadhi ya watu waliokuwa wamepuuza Mkazeni wakasema, “Oneni mtabiri yule na ndoto zake. Maafaaliyoyatabiri ni hizi pesa tunazozipata? Alitaka tufe maskini? Muone sasa, amenyamaza jii kama maji yamtungi. Anasema anaihubiria familia yake isijihusishe na biashara haramu. Biashara gani haramu hapa? Chakupata si cha kuiba.”Baada ya muda, familia nyingi zikaanza kulia. Utabiri ukaja kutokea kweli. Wadudu walikuwa niUKIMWI na joka likawa maangamizi yaliyoletwa na madhara ya UKIMWIA. Wanakijiji waliathirika nakujuta. Kituo hicho cha biashara kikawa na sifa mbaya. Watu wengi wakafa na biashara ikazidi kufifia.Mkazeni akawa anasikitishwa na matokeo ya mapuuza na tamaa za wanadamu. Kwake yeye na familiayake waliendelea kuishi vyema kinidhamu.31. Mkazeni alikuwa karimu kwa sababuA. Alitabiri mambo mengi bila chukiB. Aliwatabiria watu mambo bila kuwalipishaC. Watu wengi walimwendea kwa utabiriD. Watu wengi walimdharau lakini hakulipiza32. UKIMWI ndotoni unaweza kulinganishwa naA. Wadudu na joka kubwaB. Matrela na maderevaC. Madereva wenye wadudu33. Wanakijiji wanaposema, “Sasa nguvu zako zautabiri zinapotea” wanamaanishaA. Mkazeni si mtabiri tenaB. Wanaushuku utabiri wa mkazeniC. Hawautaki utabiri wa MkazeniD. Mkazeni hutabiri yasiyo ya kweli34. Bishara madukani ziliongezeka kwa sababuA. Watu wengi walikuja kutafuta utabiri waMkazeniB. Kulikuwa na starehe nyingi katika masokoC. Tujueni ilikuwa kituo cha mapumziko chamadereva wa matrelaD. Tujueni ilijulikana na madereva wa matrelamakubwa35. Watu wengi wa tujueni walikuwa niA. Wenye tamaa na watabiriB. Wapuuzaji na watabiriC. Wenye tamaa na malezi boraD. Wapuuzaji na wenye tamaa36. Kulingana na taarifa hii, UKIMWI uliendelezwasana na:A. Madereva wa magari na matrelaB. Wafanyibiashara wenye matrela na magariC. Madereva wapitiao katika vituo vya biasharaD. Wazazi wenye tamaa ya kupata mali37. Baada ya Mkazeni kupuuzwa tena alichukuahatua zipi?A. Alitabiri mara ya pili na kungojea matokeoB. Alibishana na wapuuzaji na kuwapamatokeoC. Aliwaangalia tu waliompuuza na kuendeleakutabiriD. Alinyamaza, akaongoza familia na kungojamatokeo38. Kutojihadhari kabla ya hatari ni sawa na:A. Kutojitayarisha kukabiliana na tatizoB. Kutoshughulika na hatariC. Kutoshughulikia matatizo yajapoD. Kutoogopa madhara ya tatizo39. Familia ya Mkazeni ilinusurika kwa kuwaA. Ilikuwa ukufundishwa kuhusu utabiriB. Haikufanya biashara na maderevaC. Ilizingatia maadili na mashauriD. Mkazeni alikuwa mtabiri40. Kichwa kifaacho zaidi kueleza kifungu hiki ni:A. Mkazeni wa Tujueni na utabiri wakeB. Asiyesikia la mkuu huvunjika guuC. UKUMWI utaangamiza watu wengiD. Mchelea mwana kulia hulia mwenyeweSoma taarifa hii kisha ujibu maswali 41 mpaka 50Maendeleo ya nchi hutegemea mchango na juhudi za kila mwananchi. Hata hivyo, ni jambo la kusikitishakuona kuwa baadhi yetu tuna fikira zisizo za kizalendo kuwa wengine ndio wanaopasa kuiendeleza nchi.Watu wa aina hii hutarajia serikali kuwafanyia hili na lile. Huwathubutu kujiuliza je, mimi nimeifanyia nininchi yangu?Inafaa tukumbuke kwamba nchi ni kama chombo cha usafiri na kila mtu ana wajibu wa kuhakikishakwamba chombo hicho kimekwenda ipasavyo. Tunahitaji kuwa na bidii za mchwa za kujenga kichuguu.Tuwe na umoja wa nyuki ambao, japo ni viumbe wadogo hudiriki kutengeneza asali ambayo huwafaa wao nakuwalisha binadamu. Ikiwa vidudu hivi vinaweza kuilisha jumuiya, sembuse sisi?Mungu amemtunukia kila mmoja wetu vipawa anuwai. Ni juu yetu kuvitumia vipawa hivi kuinua uchumiwa nchi. Tukujitahidi pamoja tutaweza kutatua matatizo mengi yanayoikumba nchi. Tukumbuke kwambakinga na kinga ndipo moto uwakapo. Wananchi katika nyanja mbalimbali hawana budi kuziimarisha nyanjahizi ili kuinua hali zao za maisha. Mathalani, wakulima watumie njia za kisasa za ukulima ili kuzalisha mazaomengi. Wakifanya hivyo, tutaweza kukabiliana na baa la njaa ambalo linawadhuru wananchi wengi.Vijana nao wana jukumu lao kwa taifa. Wewe kama mwanafunzi, unaweza kuchangia maendeleo ya nchihii kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za shule. Ujibidiishe vilivyo, si katika masomo pekee, lakinipia katika michezo. Kwa kuiendeleza michezo ya riadha na hata ya kuigiza, utakuwa umeiendeleza nchi kwakuukuza utamaduni wako. Isitoshe, unaweza kushiriki katika shughuli za kuzoa taka katika mtaa ulio karibuna shule yako. Ukifanya hivyo utakuwa umeitikia wito wa serikali wa kuhufadhi mazingira.Sehemu za mashambani zinahitaji kushughulikiwa kimaendeleo. Licha ya kuwa sehemu nyingi zinarutuba, vijana wengi baada ya kupata masomo huhiari kuhamia mjini kutafuta kazi zenye hadhi. Mashambayameachiwa wazee na bila shaka mazao yamekuwa haba. Hebu tujiulize, je, ikiwa sisi vijana tutaziachasehemu zetu na kuhamia kwingine, nani atakayeziauni? Je, hatujui kuwa chetu ni chetu na nguo ya kuazimahaifai chochote? Ni vyema tukumbuke kuwa ikiwa tunataka kusaidiwa kuendeleza sehemu zetu, ni lazima sisiwenyewe tuwe tayari kuzitumikia kwani abebwaye hujikaza. Mapenzi kwa nchi ni muhimu mno. Shimetuungane kuijenga nchi yetu.41. Maendeleo ya nchi yanahitajiA. Kushughulikia kila mara katika kilimoB. Ushirikiano wa kila mwananchiC. Kutotarajia serikali kufanya loloteD. Watu wengine kuendeleza nchi42. Watu walio na fikra za kizalendo ni waleA. Wanaotarajia kusaidiwa kila maraB. Wanaowataka wengine kushughulikiamiradi ya maendeleoC. Wasiojua wameifanyia nini nchiD. Wasiopuuza wajibu wao katika kuendelezanchi43. Nchi ni kama chombo ch usafiri kwa sabau:A. Wananchi wasipoendeleza nchi itazorotaB. Bila chombo usafiri haufanikiwiC. Wananchi wasiporudi mashambani nchiitazorotaD. Bila wasafiri nchi haifanikiwi44. Binadamu wanalinganishwa na nyuki kwaniA. Wakiwa na bidii nyingi wanaweza kujifaidiwao na wengineB. Nyuki wana umoja japo ni viumbe wadogoC. Wakiwa na umoja na bidii wanawezakujifaidi wao na wengineD. Nyuki na mchwa wana bidii za kujenga45. Katika kifungu, matendo yanayoonyesha ukweliwa methali, “Kinga na Kinga ndipo motouwakapo” niA. Vijana kuzoa taka na sote kushiriki katikamichezoB. Wote kurudi mashambani na kulima kwabidiiC. Vijana kudumisha utamaduni na kuimarishaelimuD. Ushirikiano wa nyuki na wananchikujitahidi pamoja46. Kulingana na kifungu, matatizo mengiyatatatuliwa iwapoA. Tutafanya kazi kwa pamoja bila kuzingatiatofauti zetuB. Sote tutakuwa na vipawa tofauti tofautiC. Sote tutajibidiisha katika masomo yetuD. Tutatarajia misaada kuinua hali za maishayetu47. VijanaA. Wanapaswa tu kushughulikia masomoB. Wanapaswa kusoma ili kukuza utamaduniC. Wanapaswa kushiriki kuiimarisha nchikatika nyanja mbalimbaliD. Wanapaswa kushirikiana wao kwa waokujiinua na kuimarisha kilimo48. Kulingana na kifungu maana ya kazi zenyehadhi niA. Kazi zinazolipa mishahara mikubwaB. Kazi zinazofikiriwa kuwa bora kuliko zamashambaniC. Kazi zenye marupurupu mengi kuliko zamashambaniD. Kazi za walio na elimu ya juu49. Kulingana na kifungu hiki, abebwaye hujikazaina maanaA. Unaposaidiwa lazima nawe pia ujitahidiB. Ukibebwa mgongoni usilegee kamweC. Tusitarajie kusaidiwa bila kusaidiaD. Tukiwasaidia wengine lazima tujitahidi50. Ikiwa vidudu hivi vinaweza kulisha jumuiya,sembuse sisi? Maana yake niA. Nyuki wanaweza kulisha watu wengiB. Binadamu ana uwezo wa kushirikianaC. Nyuki wana ushirikiano kuliko binadamuD. Binadamu wana nguvu za kuzalisha kulikonyuki ................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download