Athari Za Kifonolojia Za Lahaja Ya Kiamu Na Kitikuu Katika Kiswahili Sanifu

ATHARI ZA KIFONOLOJIA ZA LAHAJA YA KIAMU NA KITIKUU KATIKA KISWAHILI SANIFU

VIRGINIA WAIRIMU GAITHUMA

Tasnifu hii imewasilishwa kwa ajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

2016

UNGAMO Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijawahi kutolewa kwa mahitaji ya shahada katika chuo kingine

___________________________ Virginia Wairimu Gaithuma

_____________________ Tarehe

Tasnifu hii imetolewa kutahiniwa kwa idhini yetu kama wasimamizi walioteuliwa wa Chuo Kikuu cha Nairobi

_____________________________ Prof. Iribe Mwangi

_______________________ Tarehe

____________________________ Dkt. Prisca Jerono

_______________________ Tarehe

ii

TABARUKU Tasnifu hii naitabarukia wazazi wangu wapendwa Samuel Gaithuma na Felista Wamaitha kwa kunilea, kunipa nafasi ya kupata elimu na kunipa moyo wa kuendelea na masomo. Vilevile naitabarukia ndugu zangu George Ndungu, Martin Gitau na Mercy Waithera kwa kunipa moyo wa kuendelea licha ya changamoto zote katika safari yangu ya masomo. Pia kazi hii naitabarukia mpwa wangu Claudia aliyezaliwa katika kipindi hiki cha kuandika tasnifu hii. Mungu akupe maisha marefu.

iii

SHUKRANI Mwanzo kabisa namshukuru Mwenyezi mungu kwa kunijalia uhai, afya njema na kuniwezesha kuyakamilisha masomo yangu ya uzamili. Hakika kazi kama hii haiwezi kukamilika bila ya msaada wa watu wengine. Ningependa kuzitoa shukrani zangu za dhati kwa wote waliochangia kwa njia moja au nyingine katika ufanisi wa utafiti huu hasa wale ambao sikuwataja. Kwanza kabisa shukrani zangu za dhati nazitoa kwa wasimamizi wangu Prof. Iribe Mwangi na Dkt. Prisca Jerono ambao waliniongoza vyema kutoka mwanzo hadi nilipoikamilisha kazi hii. Daima nitawashukuru na kuwatakia heri njema na baraka za Mwenyezi Mungu kwa usaidizi na uvumilivu wao. Pia nawashukuru wahadhiri wote katika idara ya Kiswahili walionifundisha wakiwemo Dkt. Zaja Omboga, Prof. Mwenda Mbatiah, Dkt. Evans Mbuthia, Prof. Kineene wa Mutiso, Prof. Rayya Timammy, Dkt. Amiri Swaleh, Prof. Habwe na Dkt. Jefwa Mweri. Vilevile nawashukuru walimu wa shule za msingi za Wiyoni, Lamu Boys, Rasini Girls na Faza boys kwa kuniruhusu kutangamana na wanafunzi wao na kupata data iliyofanikisha utafiti huu. Hali kadhalika nawashukuru Bwana Abdurahim Bakathir na Julius Kirigha ambao nwafanyikazi katika shirika la RISSEA Mombasa kwa msaada walionipa hasa katika ukusanyaji wa data yetu. Nawashukuru wanafunzi wenzangu ambao tuliabiri pamoja katika chombo hiki na kusafiri pamoja mpaka mwisho wake licha ya changamoto zote katika mwendo huu. Nao ni Sarah, Wakesho, Lily, Dorcas, Florence, Jackline, Lavaya, Alice, Tecla, Catherine, Winnie, Braicy, Eunice, Lokidor, James, Patrick, Makori, John, Risper Seraphine, Mumo na Nyakeno. Shukrani za kipekee kwa rafiki na mwanafunzi mwenzangu Sarah Mueni kwa kukubali kuwa kiongozi wetu wa darasa. Pia namshukuru kwa kuwa pamoja nami wakati wote nilipokuwa maktabani, kuniondolea upweke na kunipa moyo wa kuendelea muda wote tulipokuwa maktabani. Shukrani za kipekee kwa rafiki yangu Cleoph ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kunihimiza kulenga juu masomoni kama yeye na pia kunifadhili kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa nimefaulu.

iv

ISHARA NA VIFUPISHO

[ ] Mabano ya fonetiki

/ / Mabano ya fonimu

+ Kuwa na sifa fulani

-

Kutokuwa na sifa fulani

L1 Lugha ya kwanza

L2 Lugha ya pili

h

Mpumuo

v

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download