SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI

KISWAHILI

4

SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI

KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE MKONDO WA LUGHA

KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE MKONDO WA LUGHA

Yaliyomo

UTANGULIZI

iv

SURA YA KWANZA: HISTORIA YA KISWAHILI

1

SURA YA PILI: FASIHI

11

DHIMA YA FASIHI

12

SURA YA TATU: NGELI ZA MAJINA

42

SURA YA NNE: USEMI HALISI NA USEMI WA TAARIFA

70

SURA YA TANO: UTUNGAJI

73

SURA YA SITA: AINA ZA MANENO

78

iii

KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI

UTANGULIZI

K unapita wakati wa kotosha Wanyarwanda walikuwa na hamu ya kujifunza lugha ya Kiswahili lakini shida ilikuwa ni ukosefu wa vitabu vinavyoandikwa katika lugha hiyo kwa ufasaha. Ikumbukwe kuwa kazi ya kuandika vitabu si jambo rahisi kwa kila mtumiaji wa lugha. Wakati huu Kiswahili kina umuhimu sana katika jamii ya Afrika na hata katika ulimwenguni kote. Hii ni lugha rahisi kuitamka kutokana na mtindo wake kama lugha nyingine za kibantu. Kitabu hiki ambacho ni "Kitabu cha mwanafunzi kidato cha nne" kinaundwa na sehemu kuu 6 ambazo ni: historia ya Kiswahili, fasihi, ngeli za majina, usemi halisi na usemi wa taarifa, utungaji na aina za maneno. Kitabu hiki kitasaidia katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule zinazofundisha lugha kikiwemo Kiswahili. Kitatilia mkazo matumizi ya Kiswahili katika maisha ya kila siku kwa wale wanaohitaji kuelewa na kutumia Kiswahili ipasavyo. Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya kuziba pengo la ufundishaji wa Kiswahili na kumaliza mahitaji ya walimu na wanafunzi. Kitabu hiki kimejaribu kuishughulikia miundo tofauti ya lugha ya Kiswahili kwa urefu na kuondoa utata unaojitokeza katika kusoma na kufundisha Kiswahili. Kitabu hiki kimeandikwa na NDAYAMBAJE Ladislas na NIYIRORA Emmanuel ambao ni walimu kutoka Chuo Kikuu cha Elimu cha Kigali. Ndani mwake tulitoa maelezo ya kila mada inayounda kitabu hiki pamoja na mazoezi yatakayowafanya wanafunzi kukua kiakili na kijamii Katika kitabu hiki tunadhamiria kuwaeleza wanafunzi namna ya kutumia historia ya Kiswahili, sarufi ya Kiswahili, fasihi pamoja na maandishi mbalimbali kwa kuendeleza maisha yao ya kesho. Pamoja na haya, maswali maridhawa ya kufanyia mazoezi yametolewa ili kumshirikisha mwanafunzi moja kwa moja na yale anayojifunza. NDAYAMBAJE Ladislas NIYIRORA Emmanuel

iv

KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE MKONDO WA LUGHA

SURA YA KWANZA: HISTORIA YA KISWAHILI

1.1. NADHARIA TETE KUHUSU ASILI NENO KISWAHILI

Nadharia tete au chukulizi hutumia kuelezea mawazo fulani aliyonayo mtafiti kabla ya kufanya utafiti. Mawazo haya huweza yakathibitishwa au yasithibitiswe. Pia haipothesia (Wamitila 2003).

Asili ya neno"Kiswahili" ni Kiarabu "Swahel" lenye maana ya ukanda wa ardhi iliyolimwa yenye miji au vijiji vilivyoko kando kando ya bahari au mto mkubwa. Kuna nadharia mbili kuhusu neno Kiswahili :

1. Nadharia ya kwanza ni ile isemayo kuwa Kiswahili ni neno lenye viambishi Kiswahel kumaanisha watu wa pwani au mwambao yaani sehemu za kando ya mto au bahari. Kwa hiyo Kiswahili ni lugha ya watu wa pwani.

2. Nadharia ya pili ni ile isemayo kwamba Kiswahili ni neno lenye viambishi Kisiwa-hila kumaanisha watu ambao ni wenye sifa ya ujanja, ukorofi n.k. Yaani watu wanaotumia Kiswahili kwa kunyanganya mali za watu (Wahuni). Kwa hiyo, kutokana na nadharia hizi mbili na uchunguzi wa historia ya lugha ya Kiswahili, tunaona kuwa Kiswahili humaanisha watu wa pwani. Watu ambao hutumia lugha yenyewe ya Kiswahili.

Baadhi ya watu hudai kwamba tunazo nadharia kadhaa kuhusu historia ya lugha ya Kiswahili lakini tukichunguza kile wanachoita nadharia, tunagundua kwamba hizo bado ni nadharia tete hazijakuwa nadharia hasa. Kuna nadharia tete nne ambazo ni muhimu.

Nadharia tete ya kwanza ni ile isemayo kwamba Kiswahili kimetokana na lugha ya Kiarabu, ya pili ni ile isemayo kuwa Kiswahili kimetokana na mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za Kibantu zilizokuwa katika Upwa wa Afrika ya Mashariki, ya tatu inasema kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyoathiriwa na lugha ya Kiarabu, ya mwisho ni ile isemayo kwamba lugha ya Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha kadhaa za Kibantu zilizokua katika Upwa wa Afrika ya Mashariki na ikaathiriwa sana na Kiarabu kimsamiati katika kukua kwake.

1

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download