BARBRO JOHANSSON MODEL GIRLS' SECONDARY SCHOOL – …



BARBRO JOHANSSON GIRLS’ EDUCATION TRUST

JOHA - TRUST WEBSITE Johatrust.ac.tz.

Kajumulo Alexander Girls’ High School P.O. BOX 744 , BUKOBA

Email: kajumulogirlshighschool@

Mob: 0767066027/0754 512947

FOMU YA MAOMBI YA KUJIUNGA NA SHULE YA WASICHANA KAJUMULO ALEXANDER KIDATO CHA TANO 2020/2021

MAHALI SHULE ILIPO

Shule ipo katika Kitongoji cha Kishasha mkabala na Kibeta English Medium Primary School (KEMPS) mjini Bukoba.

TAARIFA ZA MWANAFUNZI

Jina kamili_________________________________Tarehe ya kuzaliwa________________ Uraia__________________________Kabila ___________________Dini_______________

01. Jina la shule aliyomalizia darasa la saba__________________________________

02. Mwaka aliomalizia darasa la saba_____________________ Mkoa ______________

03. Namba ya mtihani wa darasa la saba____________

04. Anuani ya kudumu ya mwanafunzi S. L. P_________________mji__________

Mtaa/kitongoji________________wilaya_______________mkoa___________

Simu ya mkononi_________________ E – mail_________________________

05. Je anao wazazi wote wawili? (Weka alama ya √)

Ndiyo Hapana Hasiye hai ni Baba/Mama

2. AFYA

2.01 Je, ana ulemavu wowote? (weka alama ya √)

Ndiyo Hapana Taja______________________

Je ana tatizo lingine lolote la kiafya la muda mrefu linalomsumbua? (weka alama √ )

Ndiyo Hapana Taja____________________

2.02 Wasifu wa mzazi au mlezi (Aandikwe anayemtegemea katika mahitaji yake)

Jina kamili______________________________________Kazi____________________

Anuani________________________ Simu___________________________________

Saini ya mwanafunzi________________________________tarehe_____________________

3.0 Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne.

Mwanafunzi atatakiwa kuleta matokeo yake ya mtihani wa Taifa wa kidato cha

nne mara baada ya kutangazwa rasmi na baraza la mitihani la Taifa. (Results slip)

3.01 Shule ina combinations zifuatazo (Weka alama ya (( ) kuchagua combination [pic]

COMBINATIONS |HKL |HGL |HGK |HGE |EGM |PCM |CBG |PCB |PGM |ECA | |TICK (() | | | | | | | | | | | |

Saini ya mwanafunzi…………………………………………….tarehe………………………...

4.0 MALIPO YA ADA

Ada ya shule ni Tsh 3,000,000/=.(Millioni tatu tu.) kwa mwaka mzima. Ada hii yaweza kulipwa kwa awamu moja,mbili,tatu au nne kama ifuatavyo:

- kwa awamu moja Tsh 3,000,000/=

- kwa awamu mbili 1,500,000/=

- kwa awamu tatu 1,000,000/=

- kwa awamu nne atatakiwa kulipa 900,000/= 700,000/= 700,000/= 700,000/=Malipo haya yafanyike kupitia akaunti ya shule ambayo ni Kajumulo Alexander Girls’ High School nambari ya akaunti ni 027103002790 Benki ya NBC au 31806600285 Benki ya NMB.

Tafadhali tumia jina la mwanafunzi wakati wa kulipa benki ili kurahisisha uwekaji wa mahesabu (bank statement reconciliation) na kujua kwa uhakika mwanafunzi aliyelipa. Karatasi halisi ya malipo (original bank deposit slip) iletwe shuleni kwa ajili ya uthibitisho wa malipo siku ya kuwasili Shuleni haitarudisha malipo yaliyokwishafanywa iwapo mwanafunzi hatajiunga na Shule hii.

(Ufadhili kwa wahitaji hutolewa na mlezi wa shule Prof.Anna Tibaijuka)

5.0 Vifaa vinavyotolewa shuleni bure

Shule inawapa wanafunzi mahitaji ya msingi yafuatayo: sare za shule, godoro, sahani, kijiko, kikombe, kalamu, vitabu vya kiada na ziada pia shule inatoa chakula bora.

5.01VIFAA ANAVYOTAKIWA KUJA NAVYO MWANAFUNZI

a) . Chanuo, mswaki, dawa ya meno, dawa ya viatu nyeusi (kiwi), brashi ya viatu.

b) Mafuta au losheni ya ngozi, Mafuta ya nywele, Sabuni za kufulia na kuogea, Jozi moja au zaidi ya khanga au vitenge, Taulo (pedi) za kike za hedhi za kutosha kwa muhula wote, Chupi sita (6) nyeupe au nyeusi, Sidiria 3 na gagulo/skin tight nyeusi tu 4,

c) Nguo moja ya usiku (kulalia), Mashuka mawili (2) blue au pink, Chandarua, Jozi 2 za viatu vyeusi visivyo na kisigino vya darasani (maarufu kama Juma na Roza), Jozi 1 ya viatu vya kawaida kwa ajili ya J.pili na sikukuu, viatu vya michezo, rimu za karatasi 2 (ya mistari moja 1 na isiyo na mistari A4 1), Sketi nyeusi ya marinda, T – shirt nyeupe 2 na Track suti ya blue.

d) Sweta la shule upatikana katika duka la Shule kwa shilingi 18,000/=.

e) Mwavuli mdogo, Blanket, Tochi au taa ya kutumia mionzi ya jua, Taulo 1, Jozi 1 ya kanda mbili na Toilet Paper 6.

f) Pesa za matumizi madogo madogo zisizozidi 30,000/=.

g) Wanafunzi wanaosoma hesabu, Geografia na sayansi waje na scientific calculator aina ya FX-991 MS au FX-991ES, (Dissecting Kit kwa wanafunzi wa Biology wa kidato cha tano)

h) Wanafunzi wanasisitizwa kuleta masanduku madogo.

i) Kaunta book zisizopungua nane (08) za kwaya three au four. (madaftari).

j) Bima ya Afya (tunasisitiza mwanafunzi aje na kadi ya Bima ya Afya ya NHIF au aje na Tshs 5,000/= ili akatiwe bima ya mwaka mmoja.

6. Nidhamu.

Wanafunzi wote wanatakiwa kuzingatia na kutilia maanani wajibu wa mwanafunzi wa shule ya Kajumulo ambao watapewa nakala yake siku ya kuwasili shuleni. Kushindwa kufanya hivyo, kunaweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kufukuzwa shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuwahi katika kila kitu, kuwa watiifu, wanaojituma, kuvumilia tofauti za wengine na kuonesha ushirikiano.

1. ANGALIZO:

2. Wanafunzi hawaruhusiwi kuleta vyakula shuleni, vitu vya thamani kama kamera, radio, simu za mkononi na vitu vinavyoweza kusababisha ajali ya moto kama mishumaa, viberiti, taa za kandili n.k. kama ilivyofafanuliwa kwenye Wajibu wa Wanafunzi.

3. Mwanafunzi atatakiwa kusaini sheria na taratibu za shule siku ya kuripoti shule

4. Shule haipokei fedha taslimu na hairudishi ada iliyokwishalipwa.

5. Mwanafunzi mwenye matatizo ya kiafya yaliyothibitishwa na daktari aje na vielelezo

6. Shule haiusiki na gharama za macho na meno

7. Gharama za usafiri zitalipwa na mzazi /mlezi

Tafadhari rudisha fomu hii kwa kupitia anuani ifuatayo:

Kajumulo Alexander Girls’ High School P. O Box 744, Bukoba.

AU piga No. zifuatazo:-

Mob: 0767066027/0754 512947

UNAKARIBISHWA KAJUMULO ALEXANDER SHULE YA WASICHANA.

KARIBU SANA

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download