KIS 212- KISWAHILI MORPHOLOGY MAIN EXAM - Kibabii University Library

KIS 212- KISWAHILI MORPHOLOGY

MAIN EXAM - REGULAR 2ND YEAR SECOND SEMESTER- 2013/2014 ACADEMIC YEAR

Maelekezo: jibu maswali manne: Swali la kwanza ni la LAZIMA

1. (a) Fafanua dhana za mofu na alomofu kwa kutumia mifano mwafaka (alama 10)

(b) Bainisha mofu na mofimu katika maneno yafuatayo: (i) Lililopotea (ii) Kupwa (iii) Kitakachonunuliwa (iv) Vilivyotuvunjikia (v) Hawakuwapokea

(alama 15)

2. Kwa kutoa mifano mwafaka tathmini mfumo wa kimofolojia wa uainishaji ngeli za nomino

katika lugha ya Kiswahili

(alama 15)

3. Eleza jinsi ambavyo taaluma ya mofolojia inavyohusiana, inavyoingiliana na kujengana na

taaluma zifuatazo:

(alama 15)

(i) Fonolojia

(ii) Sintaksia

(iii) Semantiki

4. Kwa kutoa mifano, eleza aina mbalimbali za viambishi katika vitenzi vya Kiswahili.

(alama 15)

5. Kwa kutoa mifano, jadili mbinu zozote tano za uundaji wa maneno katika lugha ya Kiswahili

(alama 15)

6. Pambanua jinsi nomino huundwa kwa kupitia njia ya uambishaji na unyumbuaji (alama 15)

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download