Ushawishi wa Bajeti ya Afya katika Serikali ya Tanzania

SEPTEMBA 2015

Ushawishi wa Bajeti ya Afya katika

Serikali ya Tanzania

Mwongozo wa Asasi za Kiraia

Ushawishi wa Bajeti ya Afya katika Serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za Kiraia

iii

Cover photo credit: Hendri Lombard

Suggested citation: Bujari, P., and E. McGinn. 2013 Ushawishi wa bajeti ya Afya katika serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za kiraia. Washington, DC: Futures Group, Health Policy Initiative,Task Order 5.

Orodha

SHUKRANI........................................................................................................................... 2

1. UTANGULIZI....................................................................................................................... 3 1.1 Jinsi ya kutumia Kijarida.............................................................................................. 3 1.2 Mantiki ya Kijarida....................................................................................................... 4

2. MBINU NA MIKAKATI ILIYOFANIKIWA KATIKA UTETEZI WA BAJETI TANZANIA.................................................................. 7 2.1 Utambulisho wa Utetezi katika mambo ya Afya................................................... 7 2.2 Mbinu na mikakati iliyofanikiwa katika Utetezi wa

maswala ya Afya Serikalini.......................................................................................... 7 2.2.1 Mipango ya Ushawishi....................................................................................... 8 2.2.2 Kufanya kazi na wenyeji.................................................................................. 14 2.2.3 Kufanya kazi na washawishi........................................................................... 14 2.2.4 Kufanya kazi na wanachama na washindi.................................................... 14 2.2.5 Kufanya kazi na vyombo vya habari............................................................. 15 2.2.6 Ufuatiliaji wa ahadi........................................................................................... 16

3. UANDAAJI BAJETI NCHINI TANZANIA................................................................... 17 3.1. Pesa zinatoka wapi?................................................................................................... 17 3.2. Bajeti inapangwaje?.................................................................................................... 19 3.3. Jinsi gani bajeti inaandaliwa?..................................................................................... 20 3.4. Sehemu zinazopitia kwenye Utetezi wa Bajeti ya Sekta ya Afya...................... 22

3.4.1. Ngazi ya Taifa.................................................................................................... 22 3.4.2. Ngazi ya Wilaya................................................................................................ 24

4. UCHUNGUZI KIFANI ULIOFANIKIWA KWENYE UTETEZI WA BAJETI....... 31 4.1. Ushawishi wa ngazi ya Wilaya kwenye bajeti ya

serikali kuhusu Uzazi wa Mpango........................................................................... 31 4.2 Uboreshaji wa Upatikanaji wa Madawa:

Kwa kutumia njia jamii za ufuatiliaji katika kuwajibika....................................... 34 4.3. Uchunguzi kifani kwa ajili ya Kushawishi Mfumo wa

Bajeti kwa Maendeleo............................................................................................... 37

VIFUPISHO.......................................................................................................................... 40

MASHIRIKA YANAYOFANYA KAZI KWENYE UTETEZI WA BAJETI NCHINI TANZANIA................................................................................. 42

KUMBUKUMBU NA RASILIMALI................................................................................. 44

ORODHA YA MAJEDWALI NA TAKWIMU............................................................... 46

Shukrani

The USAID | Mpango wa Sera ya Afya, Task Order 5 unapenda kuwashukuru watu na mashirika yafuatayo kwa mchango wao wa thamani: Shukrani kwa Dkt. Peter Bujari, Health Promotion Tanzania na Erin K. McGinn, Futures Group, kwa ubunifu wao na utunzi wa kijarida; Bwana Simon Malanilo, Mch. James Mlali, na Jaliath Rangi kwa ajili ya michango na utafiti wao; na Molly na Jim Cameron, Lori Merritt, na Mary Brunnemer Brabble kwa umakini katika masahihisho na usanifu . Tungependa kutambua vyema mchango mkubwa wa timu iliyopitia, ambayo imehusisha wafuatao: Jasminka Milovanovic (Save the Children Tanzania Office); Edward Kinabo (Advance Family Planning/Johns Hopkins University); Dkt. Conrad Mbuya (WAJIBIKA), Manka Kway (Deutsche Stiftung Weltbevoelkerung [DSW]), Petronella Mwasandule (TUNAJALI II), na Cristin Marona (Futures Group). Mradi pia ungependa kuwashukuru watu wafuatao kwa muda wao na michango ya thamani wakati wa utafiti wa kijarida hiki: Dkt. Msengi Mwendo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe; Mustafa Sabuni, Afisa Mipango wa Wilaya ya Kisarawe; Mganga mfawidhi; Gunini Kamba, Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni; Dkt. Ezra Ngereza, Mratibu wa Afya wa Manispaa ya Kinondoni ; Simon Moshy, Afisa Mradi wa Sikika; Elinami Mungure, kutoka DSW Tanzania; Anna Nswila, Msimamizi wa mambo ya Bajeti Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (MoHSW); Jumanne Mwasamila, Mratibu wa Mfuko wa Afya TAMISEMI (Ofisi ya Waziri Mkuu?Tawala za mikoa na serikali za Mitaa). Watunzi wanapenda kutoa kijarida hiki kwa heshima ya kumbukumbu ya Tim Manchester, USAID, aliyeidhinisha kazi hii, lakini hakujaliwa kuona ukamilisho wake. Alikuwa mtu ambaye hakuchoka kuhamasisha wafadhili, viongozi wa serikali, na jamii kwa ujumla kuboresha upatikanaji wa huduma bora za uzazi wa mpango Tanzania. USAID | Mpango wa Sera ya Afya unatekelezwa na Futures Group. Unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Marekani na Tanzania kupitia ofisi ya Mpango wa Afya na Takwimu na Mfuko wa Dharura wa Raisi wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR). Maoni yaliyotolewa kwenye chapisho hili hayaakisi maoni ya Shirika la Maendeleo la Marekani au Serikali ya Marekani.

2 n Ushawishi wa bajeti ya Afya katika serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za kiraia

1 Utangulizi

1.1 Jinsi ya Kutumia Kijarida

Madhumuni ya kijarida hiki ni kuwapatia taarifa Asasi za Kiraia (CSOs) ya jinsi gani bajeti ya afya inapatikana nchini Tanzania, na kupendekeza njia kwa wawakilishi kushawishi mabadiliko. Ni njia ya kutambulisha na mwongozo rahisi kwa ajili ya utetezi wa bajeti ya afya. Machapisho mengi mazuri na ya upana mkubwa yametumika kwenye kuandaa mwongozo huu, na yanaweze kupatikana kwenye sehemu ya kumbukumbu na rasilimali kwenye sehemu ya nyuma ya chapisho hili.

Sehemu ya kwanza inaelezea mambo ya afya kama ni haki nchini Tanzania na jinsi ya mgawanyo wa serikali ulivyo kwwenye mambo ya afya kwasasa. Inatoa mwongozo kwa ufupi wa majukumu ya Asasi za Kiraia (CSOs) kwenye kuandaa bajeti ya serikali na umuhimu kwenye kuhusisha kushawishi bajeti ya afya.

Sehemu ya pili inaangalia dhana ya msingi na njia muhimu kwenye mambo ya utetezi, na inataja mbinu chache na mikakati ambayo imependekezwa kwa ajili ya Asasi za Kiraia (CSOs) Tanzania.

Wakili ni nani?

Wakili ni mtu ambaye anaongea (au kuandika) kwa umma/kwa uwazi jinsi gani vitu vipo na jinsi gani vinatakiwa kuwa. Wakili wanahamasisha mabadiliko, na mara nyingi, wanapigania hali nzuri ya wasiojiweza. Unaweza tetea kundi (kwa niaba yao), au pamoja na kikundi (kuboresha uwezo wao, au kama mwanachama wa kikundi). Wakili anaweza kuwa mtu yeyote?kijana au mzee, tajiri au masikini, aliyeelimika au asiyeelimika.

Sehemu ya tatu inatoa taarifa juu ya mfumo wa afya nchini Tanzania na mipango muhimu unayotakiwa kujua iwapo unatakiwa kushawishi mabadiliko, haswa inayohusu jinsi ya kupanga bajeti au uangalizi. Na pia inatoa taarifa ya jinsi gani bajeti ya afya ya serikali inavyopangwa na kushughulikiwa, na viashiria na muda katika ngazi ya Taifa na Serikali za Mitaa kwa ajili ya ushawishi uliofanikiwa wa bajeti ya afya.

Sehemu ya nne inahusu masomo husika ya kujifunzia kutoka kwenye Asasi 3 za Kiraia juu ya utetezi wa bajeti za serikali; mbili toka ngazi ya taifa na moja toka ngazi ya wilaya. Masomo hayo ya kujifunzia yanatoa taarifa juu ya jinsi gani ajenda za utetezi ziliandaliwa, mikakati/njia gani zilitumika, na matokeo yake. Taarifa zaidi juu ya masomo zinaweza kupatikana kwa kutumia anuani zilizotolewa.

Msomaji anaweza kupata orodha ya vifupisho, marejeo na njia, na taarifa juu ya mashirika yanayofanya kazi kwenye mambo ya utetezi wa bajeti ya afya nchini Tanzania nyuma ya kijarida hiki.

Ushawishi wa bajeti ya Afya katika serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za kiraia n 3

1.2 Umuhimu wa Kijarida

Kila mwanadamu ana haki ya kupata afya,1 na serikali ina wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa vile vitu vinavyosaidia upatikanaji wa afya zetu, kama vile maji safi, afya ya msingi, madawa muhimu, na huduma za afya. Nchini Tanzania, ahadi ya kulinda na kuboresha afya za watanzania imeanishwa kwenye Mpango wa Sera ya Afya ya 1990 (iliyopitiwa 2003), pia kwenye Mikakati ya kupunguza Umaskini (unaojulikana kama MKUKUTA) na haswa kwenye Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (I-III). Tanzania pia imejizatiti kwenye mpango wa kimataifa na makubaliano juu ya afya, kama vile Alma Ata Declaration (1978), Afya kwa wote kwa Karne ya 21 (1998), Azimio la Abuja (2001),2 the Azimio la Kampala juu ya Gharama za Afya za Haki na Endelevu (2005),3 na hivi karibuni, kwenye Azimio la Kisiasa la Rio juu ya the Rio Political Declaration on Social Determinants of Health (2012).4

Serikali pia inaonyesha kujizatiti kwake katika afya kikubwa kwa kupanga fedha za umma kwenye shughuli zinazohusu afya. Ingawa mipango ya kufadhili afya ya jamii iliongezeka mara mbili kati ya mwaka 2006 na 2012, ni asilimia 10% tu ya bajeti ya serikali ilipangwa kwa ajili ya afya, asilimia 15 chini ya ilivyopangwa kwenye Azimio la Abuja. Hii inatafsiri kwamba dola 14.905 za Marekani kwa mtu mmoja (kwa mwaka 2012), kumaanisha ni chini ya ilivyopangwa na Shirika la Afya la Dunia ya dola 54 za Marekani6 na bado ni chini ya lengo la Tanzania la dola 15.75 za Marekani kama inayoonyeshwa kwenye Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa III wa mwaka.

Mipango finyu ya ufadhili wa afya ina

Pesa za jamii ni pesa zako!

madhara mengi, ikiwa afya ni kitu cha

Pesa za serikali siyo mali ya serikali, ni kwa ajili ya wananchi. Serikali ina wajibu wa kukusanya na kuzigawa pesa za jamii kuwanufaisha watu wote kwa usawa. Kwa sababu pesa ya serikali ni mali yako, una haki ya kufahamu jinsi gani inakusanywa, inagawiwa na inatumiakaje.

msingi katika maendeleo endelevu. Nchini Tanzania, kwa kila watoto 220 wanaozaliwa, mama mmoja hufa na wengine wengi hupata madhara yatokanayo na matatizo ya uzazi. Mtoto mmoja kati ya watoto 12 hufa kabla hawajafikisha mwaka mmoja.7 Inakadiriwa kuwa mmoja kati ya wanawake 4 walio katika umri wa kuzaa wana uhitaji wa mambo ya uzazi wa mpango, na kukosekana kwa mara

kwa mara kwa huduma ya uzazi wa mpango

kunapelekea kwenye athari katika uchaguzi na upatikanaji wake. Tanzania imepiga hatua

kubwa kwenye mapitio ya UKIMWI na kuongeza vituo vya ushauri nasaha na upimaji.

Ingawa, theluthi moja ya wanawake na nusu ya wanaume hawajawahi kupimwa UKIMWI.

Kwa ujumla, asilimia 5.1 ya watanzania wenye umri wa miaka 15?49 wana maambukizi

ya UKIMWI, wenye wastani wa maambukizi ya UKIMWI mara mbili zaidi ya wanawake

asilimia (6.2%) zaidi ya wanaume asilimia (3.8%).8 Upatikanaji wa vyandarua vyenye

viwatilifu imeongezeka chini ya kampeni ya upatikanaji wa vyandarua kwa wote nchini

Tanzania, lakini kwa makadilio theluthi moja ya watanzania hawatumii (hawalali kwenye)

vyandarua vilivyotiwa dawa, na vipimo vya haraka, vinaonyesha kuwa kati ya watoto

100 walio chini ya miaka mitano wanaopimwa, tisa wana malaria.9 Wastani wa Malaria

4 n Ushawishi wa bajeti ya Afya katika serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za kiraia

Umbo namba 1: Mgao wa Bajeti kwenye Sekta ya Afya kati ya Serikali na Wahisani

Umbo namba 1: Mgao wa Bajeti kwenye Sekta ya Afya kati ya Serikali na Wahisani

Serikali

Wahisani

100%

29%

80%

60%

40%

71%

20%

47%

41%

53%

59%

0

FY 2006/07

FY 2010/11

FY 2011/12

Chanzo: Takwimu kutoka Ripoti ya matumizi ya umma (PER) ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, 2012.

unaongezeka kutokana na umri, na makadilio ya asilimia 10 kwenye sehemu za vijijini na asilimia 3 kwa sehemu za mijini.

Serikali ya Tanzania inahitaji kuweka rasilimali zaidi kwenye afya na kutumia rasilimali hizo kwa ufanisi. Uteteaji kupitia kwa Asasi za Kiraia na watu binafsi ni muhimu kuhakikisha hili linatokea, na ndo maana ya mwongozo huu. Asasi za Kiraia zina mchango mkubwa kuhakikisha serikali inawajibika katika mipango yake, na kuwafanya wafanyakazi wa serikali wanawajibika kwenye ugawaji wa rasilimali na matumizi yake. Kwa mfano, Mkakati wa Msaada wa Pamoja wa mwaka 2006?201010 unaeleza kwa muhtasari umuhimu mkubwa unaofanywa na Asasi za Kiraia katika kuwafanya serikali na wafadhili wawajibike. Kwa muongo mmoja, Asasi za Kiraia zimekuwa mstari wa mbele katika kuingilia kati kwenye mambo ya uangalizi wa bajeti na kuripoti juu ya matumizi ya umma katika nchi zote duniani ? na wanawaweza kufanikiwa. Kwa mfano, utafiti wa mwaka 2012 wa utetezi wa bajeti uliofanywa na Asasi za Kiraia nchini Uganda, Bangladeshi, na Ufilipino ilibainisha kuwa kuhusishwa kwa Asasi za Kiraia katika utetezi wa mipango ya bajeti ina ushawishi chanya katika mipango ya afya ya uzazi.11 Mifano mizuri ya utetezi wa bajeti ya afya nchini Tanzania pia imeelezwa katika mwongozo huu (angalia Sehemu ya 2 na ya 4). Pia, utetezi wa bajeti mara nyingi ni mgumu kwa Asasi za Kiraia, hii ni kutokana na uelewa mdogo katika mzunguko wa bajeti na uwazi mdogo kwa niaba ya serikali katika maandalizi ya bajeti. Mwongozo kwa jamii katika mzunguko wa bajeti wa serikali (na hapo ndipo pa kuingilia kati ili kuleta matokeo makubwa) mara nyingi unakosekana. Madhumuni ya kijarida hiki ni kuelezea kwa ufasaha jinsi gani bajeti ya afya inaandaliwa nchini Tanzania, na kupendekeza njia ambazo watetezi wanaweza kushawishi mabadiliko.

Ushawishi wa bajeti ya Afya katika serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za kiraia n 5

Asasi za Kiraia nchini Tanzania zina michango mingi tofauti katika uandaaji wa bajeti, ingawa lengo lake la msingi limejikita kwenye kushauri zaidi kupitia uwakilishi wake katika kupitia matumizi ya umma (PER) na njia kama hizo. Malengo yasiyo rasmi ni pamoja na uchambuzi wa bajeti za jamii, kutengeneza tafsiri rahisi na inayotambulika kwa wengi ya bajeti na nyaraka husika, kufanya kazi ya uangalizi, kufuatilia matumizi katika ngazi ya kata, na kutetea maboresho kwa njia ya ombi maalumu na uwajibikaji wa jumla na kwa uwazi. Wajibu usio rasmi wa Asasi za Kiraia unatambulika kuwa na athari nyingi, hasa ukishirikisha na mikakati ya kutumia vyombo vya habari na kuwahusisha wananchi.12

Jedwali la kwanza: Wajibu wa Asasi za Kiraia katika Kuandaa Bajeti

Wajibu rasmi

Kushiriki katika Mapitio ya Matumizi ya Umma na shughuli zinazoendana nazo (PER)

Wajibu usio rasmi Kuchambua bajeti ya jamii Kutengeneza tafsiri rahisi ya bajeti ili kuongeza uelewa kwa jamii Kufuatilia matumizi

Endnotes

1. Ibara ya 12 ya Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki ya Uchumi na Kijamii. 2. Wakuu wa nchi 89 walikubaliana kuweka malengo ya kutenga angalau asilimia 15 ya bajeti yao

ya mwaka kuendeleza sekta ya Afya.Wakati huohuo, walihimiza nchi wahisani kutimiza ahadi tarajiwa ya kutenga asilimia 0.7 ya Jumla ya Pato la Taifa kwa ajili ya Msaada wa Kimaendeleo (ODA) kwa ajili ya nchi zinazoendelea. 3. Inasema kuwa afya ni haki ya msingi kwa mwanadamu, ambayo inahitaji kusaidiwa na mpango endelevu na wa haki wa kifedha. Kufuatia makubaliano namba 58.31 na 58.33 ya Baraza la Afya la Dunia (WHA), inakiri kuwa matumizi ya moja kwa moja yapunguzwe na malipo ya kabla yaongezwe kwa lengo la kupunguza kudhoofisha kaya na kuendeleza kuenea kwa watu wote. 4. Baraza la Afya la Dunia namba 65.8: Nchi wanachama walionyesha makubaliano yao kisiasa ya kuboresha afya ya jamii na kupunguza kutokuwa sawa kwenye maswala ya afya kwa vitendo kwenye mipaka ya kiafya katika jamii. 5. Ripoti ya mwaka 2012 ya Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER). 6. Ripoti ya mwaka 2012 ya Mapitio ya Matumizi ya Umma. 7. Imerahisishwa kutoka vifo vya mama 454 katika kila mama 100,000 na uwiano katika vifo vya watoto chini ya miaka mitano katika kila watoto 1,000, kutokana na Uchunguzi wa Taaluma ya Takwimu za Afya Tanzania (TDHS) mwaka 2010. 8. Uchunguzi wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania (THIS) mwaka 2011?12. 9. Uchunguzi wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania, 2012. 10. Mfumo wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Serikali ya Tanzania na Wadau wa maendeleo kufikia maendeleo ya taifa na malengo ya kupunguza umaskini. Inapatikana kwenye: . Country/Tanzania/Joint-Assistance-Strategy-Tanzania-2006.html 11. Dickinson, et al., 2012. 12. Baraza la Sera na Hakielimu, mwaka 2008.

6 n Ushawishi wa bajeti ya Afya katika serikali ya Tanzania: Mwongozo wa Asasi za kiraia

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download