Printed in Tanzania 2014 - Get Value

Book Publisher:

Remili Enterprises Company P.O. Box 2311, Ihila Street Buhongwa Mwanza, Tanzania. Phone: +255 767 285 417; +255 753 455 574 Email: venerandojmilinga@

Printed in Tanzania 2014

First Print: 50 copies

Second Print: 2000 copies

ONYO: Haki zote za kitabu hiki zimehifadhiwa kwa mujibu wa sheria ya haki miliki. Hairuhusiwi kuchapisha kitabu hiki, kukinakiri kwa namna yoyote ile, hairuhusiwi kukitangaza wala kukisambaza popote bila idhini ya mwandishi au msambazaji wake Remili Enterprises Company.

Book Editor: Jacob K.Tunga

Front and Back Cover designed by: Juma V. Milinga

ISBN 978-9987- 9797-1-4

Mbinu za kupata Pesa nyingi hadi kuwa Bilionea, 2014

YALIYOMO YALIYOMO .................................................................................................ii SHUKRANI ................................................................................................iii UTANGULIZI .............................................................................................iv UJUMBE WA MWANDISHI ........................................................................v

SURA YA KWANZA1 VYANZO VYA UMASIKINI TANZANIA .......................................................1

SURA YA PILI MIRADI 66 INAYOWEZA KUKULETEA PESA NYINGI HADI KUWA BILIONEA ................................................................................................19

SURA YA TATU MAMBO 34 AMBAYO NI MWIKO KWA MATAJIRI ..................................88

SURA YA NNE MBINU ZA KUPATA MTAJI ....................................................................108

SURA YA TANO MAWAZO POTOFU KUHUSU PESA NA UTAJIRI MKUBWA. ..............121

HITIMISHO ............................................................................................130

REJEA ...................................................................................................134

Mbinu za kupata Pesa nyingi hadi kuwa Bilionea, 2014

ii

SHUKRANI

Natoa shukrani tele kwa Mungu muumba wa Mbingu na Nchi aliyenijalia kukamilisha utungaji wa kitabu hiki kizuri kikiwa cha kwanza maishani mwangu. Natoa shukrani kwa familia yangu; mke wangu Regina na watoto wangu Happiness na Neema kwa jinsi walivyonivumilia kwa muda wote nikiwa natayarisha upatikanaji wa kitabu hiki. Hii ni pamoja na Janeth na Wema binti ninaowalea nyumbani kwa jinsi walivyokuwa faraja kwa familia yote wakati wote wa kuandika kitabu hiki. Namshukuru sana rafiki yangu Jacob Kalenzi Tunga kwa kuhariri kitabu hiki chote kabla ya kuchapishwa. Mwisho Nawashukuru wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha kitabu hiki kinachapishwa na kuanza kusambazwa sokoni.

Mbinu za kupata Pesa nyingi hadi kuwa Bilionea, 2014

iii

UTANGULIZI

Hongera sana kwa Kununua kitabu hiki. Kwa Kununua Kitabu hiki umechagua kuwa tajiri, tena bilionea. Umeamua kuwa bilionea Kwa bei ndogo tu.

Kitabu hiki kinaeleza orodha ya mawazo au miradi 65 ambayo ukiitekeleza hakika unaondoka kwenye ukurasa wa watu fukara na maskini milele. Kitabu kinataja kwa mifano hai na kwa mchanganuo unaoelewaka. Miradi sahihi na makini ambayo ina mifano na mahesabu rahisi kueleweka imefafanuliwa kwa upana. Ukisoma kitabu hiki utataka uwe unakirudia mara kwa mara kukisoma kwani Hakichoshi kusoma.

Vyanzo vikuu vya umasikini Tanzania vinavyowafanya wengi wasiweze kujinasua katika tope zito la umasikini vimefafanuliwa kwa upana. Sababu kama vile Uvivu wa Kufikiri, kupenda starehe, kuchelewa kuamka,elimu mbovu, malezi mabaya, nk; vimechambuliwa kwa kina sana.

Sura ya mwisho inafafanua mbinu ambazo matajiri wakubwa huzitumia ili kupata mitaji wanayotaka. Mbinu hizo zimedadavuliwa vyema na hakika ukizisoma utapata mbinu sahihi za kupata mtaji wa mradi wowote unaoutafuta.

Aidha, miiko zaidi ya kumi inayowapasa kufuatwa na mtu yeyote anayetaka kuendelea kuwa tajiri na bilionea maisha yake yote imefafanuliwa ili kutorudi nyuma tena kifedha na kufilisika. Ukikiuka miiko hiyo, hakika hautachelewa kufilisika kabisa.

Mbinu za kupata Pesa nyingi hadi kuwa Bilionea, 2014

iv

UJUMBE WA MWANDISHI

Kwanza, Hongera kwa Kununua kitabu hiki. Nakuhakikishia kwamba ukikisoma kitabu chote hiki, hakika utaweza kuondoka kwenye umaskini si zaidi ya miaka mitano kuanzia sasa. Baada ya miaka kumi au chini ya hapo utakuwa bilionea. Wewe amini tu na uanze kazi kwa vitendo kama inavyoelezwa ndani ya kitabu hiki. Naamini kwamba baada ya kupata mbinu za kujipatia Utajiri Usiofilisika milele ndani ya kitabu hiki, ni dhahiri hautafilisika kamwe.

Kwa kusoma kitabu hiki Nakuahidi Kwamba huwezi kubakia masikini. kitabu hiki ni lazima ukisome ili uwe siyo milionea tu bali bilionea mkubwa Tanzania. Huwezi kusoma kitabu hiki usiwe bilionea kamwe!!!

Mbinu za kupata Pesa nyingi hadi kuwa Bilionea, 2014

v

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download