7.0 Je ni nyumba/majengo yapi Mawasiliano - Tanzania Revenue Authority

7.0 Je ni nyumba/majengo yapi yamesahewa kulipa kodi ya majengo?

Majengo yaliyosamehewa kodi ya majengo ni: a) Nyumba kwa matumizi ya mheshimiwa Rais b) Majengo yanayomilikiwa na kutumiwa na serikali kwa matumizi ya umma c) Majengo yanayomilikiwa na Taasisi za dini ambayo hayatumiki kwa shughuli za biashara au kiuchumi kwa kujipatia faida/ kipato d) Maktaba za umma na majengo ya makumbusho e) Makaburi na nyumba za kuteketeza Maiti. f) Majengo ya kuongozea ndege ya umma na majeshi isipokuwa majengo mengine yenye shughuli tofauti na hizo g) Majengo yenye maeneo ya viwanja vya michezo vinavyotumika kwa matumizi ya Taasisi za elimu. h) Majengo ya shughuli za meli i) Majengo yanayomilikiwa na asasi zisizo za Kiserikali (non- profit organisation) yasiyotumika kwa shughuli za biashara au kujipatia faida/ kipato. j) Majengo ya yanayomilikiwa na Serikali. Taasisi za Serikali na Taasisi nyingine za aina hiyo yasiyotumika kwa shughuli za biashara au kujipatia kipato/faida. k) Nyumba/Majengo yanayomilikiwa na serikali za Mitaa na Taasisi zake ambazo hazitumiki kwa shughuli za biashara au kujipatia kipato/faida. l) Nyumba moja ambayo ingepaswa kulipiwa kodi ya majengo ambayo inamilikiwa na kuishi mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka sitini (60) au nyumba anayoishi mlemavu ambaye hana kipato chochote. m) Majengo yoyote ambayo waziri mwenye dhamana ataamua kuyatolea tangazo kwenye gazeti la serikali.

Mawasiliano

Tembelea ofisi ya TRA iliyo karibu nawe au

Kituo cha Huduma kwa Mteja Namba za bure: 0800 780078 0800 750075

WhatsApp: +255 744 233333 Facebook: tratanzania Twitter: @tratanzania Instagram: @tratanzania

Barua pepe: huduma@tra.go.tz Mamlaka ya Mapato Tanzania Postcode: 28 Edward Sokoine Drive

11105 Mchafukoge Ilala CBD

S.L.P. Box 11491, Dar es Salaam Simu: +255 22 211 9591-4, +255 22 2127080

Tovuti : tra.go.tz

Ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa TRA: Piga simu +255 689 122 515 SMS: +255 689 122

516

Kufichua wakwepa kodi Piga simu: +255 22 2137638, +255 784 210209

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

TANZANIA REVENUE AUTHORITY

UTOZAJI NA UKUSANYAJI KODI YA MAJENGO

Julai, 2020

1.0 Utangulizi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina jukumu la kusimamia na kukusanya kodi ya majengo kuanzia Julai 1, 2016 kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya utozaji Kodi ya Majengo Sura 289, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura 290 na Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Sura 399. Hii imeainishwa kwenye Sheria Fedha ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 na Mabadiliko ya Sheria mbalimbali (The Written laws (Miscellaneous) Amendments Act No. 2 Februari, 2019.

2.0 Maana ya kodi ya Majengo

Kodi ya majengo ni tozo kwa mujibu wa sheria kwenye majengo/nyumba ambazo zimekamilika.

3.0 Kiwango cha kodi

Viwango vya malipo ya kodi ya majengo vimepangwa kwa kuzingatia aina na mahali jengo lilipo kama ifuatavyo:

(a) Kwa Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji,

(i) Shilingi. 10,000/= kwa jengo kwa nyumba ya kawaida katika kiwanja chenye jengo moja linalotumika.

(ii) Shilingi 10,000/= kwa kila jengo la nyumba ya kawaida linalotumika lililopo ndani ya kiwanja kimoja. ( mfano kama kuna nyumba zaidi ya moja kila moja itatozwa sh. 10,000/=)

(iii) Shilingi 50,000/= kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa kwa maeneo ya Halmashauri za Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji.

Angalizo: Majengo ya ghorofa yenye wamiliki tofauti kwa kila ghorofa chini ya Sheria ya Unit Titles yatatozwa kodi ya jengo kwa kila ghorofa kulingana na umiliki. Hii ina maana kwamba kila mmiliki atalipa sh. 10,000/= kwa unit anayomiliki.

(b) Kwa Halmashauri za Wilaya kodi ya Majengo itakuwa: -

(i) Shilingi 10,000/= kwa jengo kwa nyumba ya kawaida. Inayotumika. Iwapo kiwanja kina nyumba zaidi ya moja basi jengo lenye thamani ya juu ndilo litakalohesabika na kutozwa sh. 10,000/= tu.

(ii) Shilingi 20,000/= kwa nyumba ya ghorofa katika maeneo ya Wilaya. Angalizo:

? Kwa Halmashauri za Wilaya maeneo ya kutoza ni yale yaliyoko ndani ya mipaka ya makao makuu ya Wilaya na Mamlaka za Miji tu.

? Mwisho wa kulipa Kodi ya Majengo ni tarehe 31 Disemba ya kila mwaka

4.0 Majengo yasiyotozwa kodi

Kibanda cha Udongo, nyumba za Nyasi na makuti na nyumba za matope na udongo, na zinazofanana nazo.

5.0 Jinsi ya kukadiria Kodi ya Majengo

Kuna njia mbili za kujikadiria kodi ya majengo nazo ni njia ya simu ya mkononi na njia ya tovuti ya TRA.

5.1 Njia ya Simu yako ya mkononi Ili kupata namba ya kumbukumbu (Control number) itakayotumika wakati wa kufanya malipo, hakikisha una namba ya Jengo au Namba ya Mlipaji (Payer's ID) inayopatikana kwenye hati ya madai (Demand Note) namba hii siyo TIN kisha fuata yafuatayo:

? Piga *152*00#. ? Chagua Namba 5 - TRA. ? Chagua Kodi za Majengo. ? Chagua namba 1 au 2 kulingana na taarifa

ulizonazo (Namba 1 ambayo ni namba ya Jengo lako au namba 2 ni namba ya Mlipaji) na endapo jengo lako halijasajiliwa na TRA, tembelea ofisi yoyote ya TRA iliyopo karibu nawe ili kupata ankara yako. ? Utajua kiasi unachodaiwa pamoja na namba ya kumbukumbu (Control number).

5.2 Njia ya tovuti ya TRA

? Tembelea tovuti ya TRA (tra.go.tz)

kisha bofya "Huduma za mitandao" kisha

chagua "Usajili wa majengo".

? Ingiza namba ya jengo, mfano

KMC00114XXX au namba ya Mlipaji

(Payer's ID). Kumbuka namba hizo

hupatikana kwenye Ankara ya malipo

uliyoipata toka TRA mwaka uliopita, na

endapo jengo lako halijasajiliwa na TRA,

tembelea

ofisi yoyote ya TRA iliyopo

karibu nawe ili kupata ankara yako.

? Kisha bofya kitufye cha "Kadiria Kodi".

? Utajua kiasi unachodaiwa pamoja

na namba ya kumbukumbu (Control

number).

6.0 Jinsi ya kufanya Malipo

Unaweza kulipa kupitia tawi lolote la Benki ya NMB au CRDB popote nchini au kwa njia ya M-pesa, T-Pesa, Airtel-Money, Tigo-pesa au Halo-pesa.

? Fungua Menyu ya M-pesa, T-Pesa, AirtelMoney, Tigo-pesa au Halo-pesa kisha lipa kulingana na mtandao wako.

? Chagua Lipa Bili. ? Kisha chagua Malipo ya Serikali. ? Ingiza namba ya kulipia malipo (Control

number), mfano. 9910XXXXXXX. ? Weka kiasi cha pesa kulingana na kiasi

unachodaiwa kwenye ankara yako ya malipo. ? Weka namba yako ya siri. ? Thibitisha malipo. ? Utapokea ujumbe mfupi wa taarifa wa muamala ulioufanya unaosema "Malipo yamepokelewa kwenda Tanzania Revenue Authority".

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download