JunI 16, 2005 Gaudensia:Aishi kwa kuponda mawe

"Kutunza yatima ni jukumu letu wote"

JunI 16, 2005

Gaudensia:Aishi kwa

kuponda mawe

NA JOSEPH KITHAMA

Akiwa na umri wa miaka minne na nusu na mtu wa kuvutia, Bi Gaudensia Chuki alitarajia kufaidi upendo wa wazazi haki ya kucheza michezo ya kitoto na haki yake ya kimsingi ya elimu, inayotambulika kimaitaifa.

Hata hivyo, mtindo wa maisha wa Gaudensia, mkazi wa Isamilo katika Wilaya ya Nyamagana, ni ukanusho wa kweli wa haki zote za msingi zinazofurahiwa na watoto wa rika lake kila mahali duniani.

Mikono yake nyororo haijapata kumgusa mwanaserere au mchezo wa kompyuta kwa ajili ya watoto na badala yake, wakati wa umri mchanga wa miaka mitatu, Unaiwe Perusi Yusufu (56) alimpa Gaudensia nyundo ndogo ya kuvunjia mawe.

"Alianza kuvunja mawe kwa ile nyundo ndogo lakini hivi sasa anatumia nyundo kubwa zaidi, amezoea," bibi yake, anayeongoza familia ya watoto watatu waliotelekezwa; na mama yake aliye mgonjwa, alisema.

Kwa Gaudensia kuvunja mawe ndio uhakikisho pekee wa maisha. Hakuchukulii kama mfanyishaji kazi watoto, ambako kumeharamishwa na Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO), lakini kama njia ya kujikimu kwa kijungu jiko.

Gaudensia huvunja mawe kiasi cha kutosha kujaza mawe galoni mbili zilizokatwa sawa kila siku, pamoja na kaka zake wakubwa na bibi yao ambaye lazima avunje mawe kujaza ndoo kumi na mbili katika vita vya kuwafanya watoto waliotelekezwa waishi katika nyumba ya matope kwenye miteremko ya milima ya Isamilo.

Familia hiyo yatima ambayo inaishi katika matatizo yaliyokithiri inabidi ivunje mawe kila siku kujaza lori na kuuzwa kwa Tsh. 30,000. "Kwa kawaida, tunauza ndoo za mawe yaliyovunjwa kwa kati ya Tsh. 200 na Tsh. 400, ili walau tupate pesa chache za kununulia unga na dagaa,"

Gaudensia alisema. Baba alimtelekeza Renatus Tito

(13), Lucas Peter (10) na Gandensia miaka kadhaa iliyopita kwa sababu alizozijua mwenyewe. "Baadhi ya watu wanasema hivi sasa anaishi Dar es Salaam. Nani anajua! Wala hatuelewi aliko.

Familia hiyo haina chanzo chochote kingine cha kipato ila kuvunja mawe. Ni kaya isiyo na ardhi inayoongozwa na bibi asiye na uwezo wa kifedha, wa kukodi sehemu ya kulima, ambayo inagharimu Tsh. 30,000 kwa nusu ekari.

Soko la mawe yaliyovunjwa halina uhakika siku zote. Kunapokuwa na kazi ya ujenzi, familia inahakikishiwa mahali pa kuuzia mawe yaliyovunjwa, kama ilivyo hivi sasa Isimalo ambako inatengenezwa barabara ya changarawe.

"Katika nyakati kadhaa, tunashuka hadi Tsh. 200 kwa ndoo ya mawe yaliyovunjwa kutokana na ukosefu wa soko la kutegemewa Isamilo, Kata ya pekee ya Mwanza, yenye mchanganyiko wa watu wakwasi na wale wanaoishi katika mazingira magumu sana, lakini ambao wanaelekea kujali kidogo kuhusu tabaka linaloishi katika hali ngumu.

Familia hiyo haiwezi kumudu gharama za matibabu ila vidonge vya panadol, ambavyo ni vya kupunguza maumivu tu. "Tunamwomba Mungu kwa dhati atunusuru tusiugue," bibi alisema, akifunga mikono yake kwa kukata tamaa.

Karibu tu, kuna bibi mwingine, Bi Sawata Maye (50), ambaye peke yake, anawalea watoto saba wanaotoka kwenye familia mbalimbali zinazohusiana naye.

Katika hawa watoto wenye umri wa kati ya miaka miwili na 13, watoto watatu walishindwa hata kujiandikisha elimu ya bure inayotolewa na MEMKI kwa vile wao ni maskini mno kumudu kununua hata sketi ya Tsh. 2000.

Wenzi wao watatu tofauti ambao ama walikufa kwa UKIMWI au waliwatelekeza tu watoto wao kwenye

Gaudensia Chuki akiponda mawe, kama njia pekee ya kuishi

nyumba ya bibi kuchota maji kujaza kati ya mapipa mawili au matatu kila siku ili kupata Tsh. 3,500 ili kuhakikisha kwamba watoto wanaishi katika hali ya uzoefu wanaokabiliana nao.

Ingawa mvua zinazoendelea ni ishara njema kwa watu wengi, lakini kwa Sawata, ambaye kuishi kwake kunategemea uuzaji maji, mvua hizo zinayatishia maisha ya watoto wake wanaoishi katika mazingira ya hatari.

Mtoto huyu ameweza kuhudhuria shule baada ya kupewa suruali ya mtumba na Msamaria Mwema, alisema bibi ambaye huyalisha matumbo ya watoto wote waliomzunguka kwa kuuza maji kutoka kwenye bomba lililofungwa na mkazi wa Isamilo mwenye hali nzuri.

Bi Christine Mashiku, Afisa Mtendaji wa Kata ya Isamilo, anasema

watu wenye hali nzuri Mwanza

wanaishi Isamilo, eneo lililojitenga

ambalo linaweza kufananishwa na

Oysterbay, Dar es salaam. Lakini Kata

hiyo pia ni makazi ya watoto 500

wanaoishi katika mazingira ya hatari

sana (MVC), chini ya umri wa miaka

18, kwa mujibu wa utafiti wa MVC

uliofanywa Januari 2005.

Kata ya Mwanza ina watoto

wanaoishi maisha ya hatari sana ina

asilimia 6.3 ya karibu watoto 15,000

walio chini ya umri wa miaka 18

iliyozungukwa na mawe.

Changamoto

zilizobainishwa

ambazo watoto wanaoishi katika

mazingira magumu, wanakabiliana nazo

Isamilo ni pamoja na vitu vya msingi:

chakula, malazi, ukosefu wa elimu,

ukosefu wa upendo, magonjwa sugu na

kujihusisha na uhalifu.

Utafiti wa Benki ya Dunia wa hivi karibuni katika Tanzania, Uganda na Zambia umegundua kwamba mababu na mabibi walifanyiza aina moja pekee kubwa kabisa inayowatunza yatima. Wazee wanauza ardhi, mali, wakiwemo ng'ombe na mali nyinginezo katika harakati za kupata mahitaji yao wenyewe yaliyo muhimu, na kuwatunzia wajukuu wao.

Tarakimu za hivi sasa duniani zinakadiria kwamba watoto milioni 16 walio chini ya umri wa miaka 15 wanapoteza ama mmoja wa wazazi au wazazi wote wawili kutokana na UKIMWI, na watoto milioni 40 wengine watawapoteza wazazi wao katika miaka 10 mingine ijayo.

Mtoto anahangaika kutunza wadogo

Katarina Mayala, akiwa karibu kutoa machozi wakati akielezea namna mama yao alivyo watelekeza huko Kirumba Mwanza. Nyuma ni kibanda walichoa azimwa na masamaria mwema

Kibanda cha matofali ya udongo, kisicho na madirisha na kuezekwa mabati yaliyoshikizwa kwa mawe yaliyosambaa paani kipo Mwanza karibu na kaburi la marehemu baba wa watoto watatu waliotelekezwa na mama yao.

Yawezekana marehemu baba huyo akawa amepumzika kwa amani katika makaburi ya familia yaliyopo jirani, lakini maskini watoto hao watatu wanahangaikia maisha yao ndani ya kibanda hicho walichopewa msaada na msamaria mwema bada ya kubomoka kabisa kwa kile cha kwanza, kilichokuwa cha bibi yao ambaye pia ametangulia mbele ya haki.

Miaka mitatu tu baada ya kifo cha baba yao mpendwa, Katarina Baliba (17), Mayala Baliba (13) na Emmanuel Baliba (11) walitupwa Kibuhoro katika Kata ya Kirumba na mama yao aliyekimbilia Nyegezi kuolewa na mume mwingine.

Mara chache sana huwatembelea watoto wake akiwa mikono mitupu, na kuwaacha kama walivyo bila hata ya dalili ya huruma, majirani wa watoto hao walieleza mbele ya Katarina aliyekuwa akibubujikwa na

machozi. Katarina alilazimika kubeba jukumu la

kuongoza familia ya watoto watatu tangu alipokuwa na umri wa miaka 14, bila ya msaada wowote wa fedha za kuendeshea maisha yake na ndugu zake wawili wa kiume.

Kumbukumbu ya majuto na uchungu mama huyo aliyomwachia Katarina ameshindwa kabisa kuivumilia. "Kila tunapomtembelea Katarina, anatutia uchungu na kutufanya tulie' alisema kwa kuomboleza Bi. Iluminata Mwita, Ofisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Mwanza, wakati Rose Ahmed, Mwanamke mwingine aliyetusindikiza kwa watoto waliotelekezwa alikuwa akitokwa na machozi.

Katarina hakwenda shule yoyote ya msingi kwa sababu alichukua majukumu yote ya mama yake. Wakati fulani alilazimika kuwaachia ndugu zake kitanda na akalala chini, ambako kulikuwa kumelowa na mvua.

"Wakati mwingine tunalazimika

kukihama kibanda chetu usiku wa manane

ili kuokoa maisha yetu kutokana na mabati yaliyoshikizwa ambayo yanaweza kuzolewa na kimbunga au kuvuja wakati wa mvua," alisema Katarina, huku akilia kwa uchungu.

Kama vile kisa kisicho mwisho cha mateso ya moyo waliyonayo watoto waliojikuta kuwa wametelekezwa hakitoshi, Katarina alilazimika kuacha masomo katika shule ya Ufundi stadi mjini Mwanza alikotaka kusomea kuunga vyuma, kutokana na kuumwa.

Watu wenye moyo wa upendo wa Mwanza wanatafuta uwezekano wa kumfadhili Katarina akachukue masomo ya ufundi Cherehani yatakayomfaa kutokana na afya yake. Idara ya Maendeleo ya Jamii inaratibu michango ya kumsaidia binti huyo.

Kusema kweli maisha ya watoto hao watatu yanategemea msaada wa chakula wanaopewa na taasisi ya kikatoliki, iitwayo SHARON. Shirika hilo la misaada ndiyo dhamana pekee ya maisha yao.

Siku ya Mtoto Wa Afrika imekuwa ikisherehekewa tokea mwaka 1991, kwa madhumuni ya kuleta mwamko katika jamii kuhusu mambo yenye athari kwa watoto. Nchini Tanzania maadhimisho ya siku hiyo yamekuwa yakiwajumuisha watoto. Ujumbe wa mwaka huu: "Kutunza yatima ni jukumu letu wote"

2

Mahojiano na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania

Bw. Rodney Phillips, kuhusu hali ya yatima nchini

SWALI:

Mababu

na

mabibi, ambao ndilo kundi moja

kubwa la watu wanaolea yatima

nchini Tanzania wanawezaje

kusaidiwa?

JIBU: Tatizo la VVU/UKIMWI

karibu limemaliza kizazi kizima cha

wazazi na walezi wa watoto. Hivi sasa

tunawaona mababu na mabibi ambao nao

pia ni wagonjwa wakiwalea wajukuu zao.

Kaya zinazoongozwa na mabibi na

watoto wengine, ziko katika hatari

kubwa sana. Hivyo, walezi wa yatima na

walio katika hali ya hatari sana wanahitaji

msaada wa haraka. Ukubwa wa tatizo

lenyewe unahitaji mtazamo wa kijamii.

Jamii hazina budi zijihamasishe na

kujipanga zenyewe kuona jinsi

wanavyowasaidia yatima na watoto

wengine walio katika mazingira

magumu. UNICEF husaidia ubainishaji

wa watoto walio katika mazingira ya

hatari kabisa katika jamii kadhaa kwa

kuhamishia taslimu na vifaa moja kwa

moja kwenye jamii hizo.

SWALI:

UNICEF

inaisaidiaje Tanzania kukabiliana na

tatizo la zaidi ya yatima milioni

mbili?

JIBU: Kimsingi jukumu la kuwalea

yatima ni la uongozi wa serikali

ikisaidiana na Vyama vya Kiraia na

Mashirika ya Kijamii. Wizara ya Kazi,

Maendeleo ya Vijana na Michezo

imeanzisha mpango bora kabisa wa

utekelezaji wa jinsi ya kuwasaidia yatima

nchini. UNICEF itakuwa ikisaidia

utekelezaji wa mpango huu wa

utekelezaji, na uhamasishaji wa rasilimali

zitakazohitajika.

SWALI:

Je, Malengo ya

Maendeleo ya Mileniam kuhusu

Watoto yanatekelezeka Tanzania

ambako VVU/UKIMWI huua watu

wengi?

JIBU: VVU/UKIMWI wenyewe ni

lengo la milenia, lengo Na. 6 ?

lililopangwa kidunia kwa kila nchi.

Tanzania inapaswa ipange malengo yake

halisi, ambayo si lazima yawe ndani ya

muda wa malengo ya dunia. Malengo ya

hivi karibuni lazima yaakisi rasilimali

zilizomo nchini, na kuhusisha miaka

mitatu hadi minne ijayo. Hili litasaidia

maendeleo ya viashiria vya ufuatiliaji

vilivyo sahihi zaidi, na uwajibikaji

mkubwa zaidi wa kisiasa.

SWALI:

UNICEF

inaisaidia serikali ya Tanzania katika

kuwalinda watoto dhidi ya

unyanyasaji, unyonyaji na nguvu?

JIBU: Hilo ni eneo nyeti! Si

kwamba ni afya na elimu ya watoto tu

ndiyo muhimu, bali hata uelewa wa

kitaifa wa vitendo dhidi ya unyonyaji,

utekelezaji, matumizi ya nguvu na

unyanyasaji wa watoto. Uelewa

utawawezesha watoto kuzijua haki zao.

Mifumo ya kisera na kisheria

inayoshughulikia uvunjaji wa haki za

mtoto haina budi kuharakishwa na

kutekelezwa. UNICEF inaisaidia serikali

katika uendelezaji.

Sheria ya Watoto, ambayo itaimarisha

ulinzi wa watoto, balehe, na vijana

SWALI:

Ni njia ipi iliyo

bora kuwashughulikia yatima

Tanzania ? kuishi na ndugu au

katika nyumba za yatima?

JIBU: UNICEF haiungi mkono

nyumba za yatima kama njia ya kwanza

ya kutatua tatizo. Ni vema kwa yatima

kuishi na ndugu zao, katika jamii.

Tunajaribu kuwasaidia kupitia walezi wao

katika kaya za jamii. Nyumba za yatima

zenyewe zaweza kuwa chanzo cha

matumizi mabaya ya mtoto.

SWALI:

Matarjio

ya

muda wa kusihi yanapungua, hasa

kutokana na HIV/UKIMWI. Je,

Tanzania ina uwezekano wa

kubadili hali hiyo kupitia

uboreshaji wa lishe na

huduma za afya?

JIBU: Ndio, lishe na afya ni

muhimu katika kuongeza

matarajio ya muda wa kuishi,

lakini pia elimu, ambayo ni

chanjo ya kijamii dhidi ya

VVU/UKIMWI. Tanzania ina

utashi wa kisiasa wa kuongeza

matarajio ya muda wa kuishi

kwa watu wake, ikitumia

rasiliamli zake. Iwapo serikali,

vyama vya kiraia na Asasi zisizo

za Kiserikali zikifanya kazi kwa

karibu, wanaweza kupata njia ya

kubadili hali ya kushuka kwa

matarajio ya muda wa kuishi.

Mpango wa sasa wa kuongeza

uchumi na kupunguza umaskini

? MKUKUTA ? unatupa

misingi ya kuwa na matumaini

si UNICEF tu bali mfumo wa

UN kwa ujumla unaunga

mkono malengo na mikakati ya MKUKUTA, katika kupanua Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Mr Rodney

ubia kwa watoto.

Phillips akifurahi na watoto

Kwa nini Watanzania wanapendelea kutoa michango

mikubwa ya arusi kuliko kusaidia elimu ya watoto?

Yafuatayo hapa chini ni madondoo ya

watu wa aina mbalimbali kutoka Dar es

salaam na Zanzibar.

Bwana Barabona Thomas Morongo,

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la

Watu

Wanaopambana

na

VVU/UKIMWI

(WAMATA),

anakumbuka jinsi arusi aliyohudhuria

hivi karibuni ilivyotumia mamilioni ya

shilingi zilizochangwa na watu

wachache wenye uwezo, Dar es salaam.

Sherehe ya arusi hiyo ilikuwa na

orodha ya vyakula vya ziada, kama vile

uji, maziwa na vingine, ambavyo

baadhi yake wageni hata hawakuvionja.

Bwana Morongo anasema kwamba

baadhi ya watu waliochangia zaidi ya

shilingi milioni moja wakati wa

maandalizi ya arusi hiyo wana ndugu

na yatima wanaoishi katika hali mbaya,

pembeni mwao.

Bw. Morongo anadhani kwamba

msimamo wa kuchangia arusi za

kifahari badala ya kuwasaidia watoto

wanaoishi katika mazingira magumu

unatokana na urithi wa ujamaa wa

kiafrika.

"Ujamaa ulipandikiza katika vichwa

vya watu mawazo mabaya kwamba

watoto ni mali ya serikali. Kwa hiyo,

serikali ndio asasi ya pekee

inayotarajiwa kuwahudumia."

Anatoa mfano wa mikoa ya Kagera

na Kilimanjaro, ambayo haikuathiriwa

na urithi wa ujamaa kwa kiwango

kikubwa, akizingatia kwamba katika

mikoa hiyo watu wengi walifanikiwa

kuwapeleka watoto wao shule,

wakitumia pesa zilizochangwa na jamii.

Dkt.Mushy Conrad anasema

kwamba watu walio wengi

wanachangia zaidi kwenye arusi kuliko

ustawi wa yatima kwa ajili ya fahari

kuu wanayoipata wanapoahidi kiasi

kikubwa cha fedha mbele ya wenzao.

"Wanadhani kuwachangia yatima ni

mpango wa muda mrefu ambao hauna

budi ushughulikiwe na serikali.

Conrad anasema, kwa kweli

waunda sera wengi na baadhi ya

wanajamii wasiowajibika walipata

elimu yao bure. "Iwapo wao

walisaidiwa kwa nini wasiwasaidie

wengine? "Conrad anauliza.

Rose Muthamia, 20 mkazi wa

Mwanayamala anahusisha na tabia ya

kujionyesha, wahusika wakitaka kila

mtu azingatie uwezo wao. Shauku

nyingine ambayo Muthamia anaitoa ni

ile ya kuamini kwamba yatima ni

wajibu wa ndugu wa yatima hao,

wakisahau kwamba baadhi ya ndugu

wa yatima ni maskini wa kutupwa.

Kula, kunywa na kufanya sherehe ni

shughuli za kijamii zinazopendwa na

Watanzania walio wengi anasema John

Mujulizi 34, mfanyabiashara wa Jiji, na

kwamba wachangiaji wa starehe za

arusi wanasimuliwa na hujifurahisha

kwenye starehe ya arusi.

Anasema kwamba kwao michango

ya sherehe za arusi hatimaye hutumika

kwenye tafrija ikilinganishwa na

vitendo vya kumsaidia yatima ambaye kutoka kwake hakuna hata mtu mmoja anayenufaika moja kwa moja.

Hata hivyo, Mujulizi anasema kwamba wale ambao kwa kawaida husita kuwasaidia yatima wakati mwingine huwa sahihi kwani siku hizi watu wanaendesha magari ya posh na kuishi katika nyumba za kifahari chini ya mwamvuli wa yatima. Vitendo vya aina hiyo huwakatisha tamaa watu walio tayari kuwasaidia yatima.

"Wakati mwingine, fedha wanayopewa yatima inakosa mshindo kwa vile inatapeliwa na watu wachache wasio waaminifu katika jamii," anasema akiongeza kwamba hakuna mtu atakayekuwa tayari kuwaona watu wengine wakifaidi maisha kwa pesa zilizotolewa kuwasaidia yatima wakati

watoto wao. Katika shule za kulipia visiwani wazazi wachache sana hufikiria kuwapeleka watoto wao kwenye shule za kulipia, za Msingi au Sekondari na badala yake hutegemea sana shule za umma ambazo hutoa elimu ya bure hadi ngazi ya sekondari.

Kwa bahati mbaya, shule za umma zinakosa mahitaji muhimu, kama vile madawati, vitabu vya rejea na wafanyakazi wenye uwezo.

Wakati ambapo unawekwa mkazo mdogo sana wa juhudi za kuchangisha pesa kugharimia elimu Zanzibar, familia nyingi zinatumia kiasi kikubwa cha pesa kugharimia maandalizi ya sherehe za arusi.

Michango hiyo wala haiwasaidii wanandoa wapya, bali watu wanaohudhuria tafrija.

mahitaji mbalimbali ya mavazi huongezeka, ndivyo ilivyo kwa wanawake wa Zanzibar kutaka mavazi mapya wakati wa sherehe ya arusi.

Wanawake wa Zanzibar wako nyuma sana kielimu, ikillinganishwa na wanaume, lakini ndio watumiaji wakuu wa kipato cha familia katika sherehe nyingi za arusi ambazo wanaume hawana nafasi nazo.

Lakini awali ya yote swali la msingi linabaki kuwa kwa nini wazazi, ndugu na wanaume huwekeza sana katika sherehe za arusi na wakati huohuo wakifumbia macho sekta muhimu kama vile elimu.

Ali Uki ni mwandishi wa habari wa Zanzibar na anadhani jamii inahitaji kubadilika iwapo Zanzibar inataka kuipa sekta ya elimu kipaumbele.

Watoto walio katika hali ngumu: Kwanini picha kama hii ya kusikitisha haiwagusi Watanzania wanaopenda arusi za ulimbwende

ambapo watoaji wanalazimika kujikamua ili watoe msaada.

Hata hivyo, anayapa changamoto mashirika yaliyosajiliwa au wanaojitolea wakidai kwamba yanawasaidia yatima kuwa wakweli na kujitolea kwa wito huo lakini si kuzitumia kwa kujinufaisha.

Huko Zanzibar, hivi sasa ni marufuku kuchanga pesa kwa ajili ya arusi au kuandaa sherehe ghali kwa watu ambao ndio kwanza wameoana. Hata hivyo, inapokuja kwenye kugharimia elimu, ni vigumu kuwa na mipango kama hiyo.

Wakati ambapo kupata elimu ya msingi na ya sekondari kunabaki kuwa suala muhimu kabisa, miongoni mwa wazazi Zanzibar, hapa ni vigumu familia kufikiria kufanya mpango wa kuchanga fedha kwa ajili ya kuwalipia

Kiasi kikubwa cha michango ya kifedha kwa ajili ya arusi visiwani hugharimia mavazi ya gharama kubwa kwa ajili ya wanawake wanaohudhuria sherehe na mapambo mengine, lakini ni kiasi kidogo sana kinachotumika kwa viburudisho na vinywaji.

Sherehe zinabakia kuwa miradi yenye kuleta faida kwa wanawake kununua au kuzionyesha nguo zao za gharama kubwa, wanandoa wapya au wanandoa watarajiwa wakipata faida ndogo sana ya vitu.

Tanzania Bara hali ni tofauti sana. viburudisho na pombe huchukua kiasi kikubwa cha fedha iliyochangwa kwa ajili ya sherehe ya arusi na kiasi kidogo huelekezwa kwenye ununuzi wa nguo kwa ajili ya maarusi wapya.

Kama ilivyo wakati wa siku kuu ya Noeli Tanzania Bara, wakati ambapo

Alisema kwamba kutumia fedha nyingi kwenye sherehe za ndoa, ambazo ni vigumu kudumu, ni upotevu wa rasiliamli.

Anasema sasa wakati umefika kwa wazazi wa Zanzibar kuwekeza kwa watoto wao na anasema mojawapo ya mambo ya kufikiriwa ni kutumia fedha kwa ajili ya elimu.

Bw. Uki anasema miundo-mbinu ya elimu iliyopo visiwani haitoshelezi, kwa vile kiwango cha asasi hizi za umma hakiridhishi kabisa.

Ni maoni yake kwamba mchakato halisi wa uchagiaji wa arusi ndio unaounganisha utegemeano wa kifamilia au kiunganishi miongoni mwa wanandugu wa karibu.

Huu ndio utamaduni anaosema kila mtu miongoni mwa marafiki na ndugu na kila mtu katika familia anahisi

anapaswa kufuata.

Anasema kuchepuka kutoka

kwenye kaida za desturi humweka

mchepukaji katika mgongano na jamii,

kukabiliana na vizuizi vingi licha ya

kumweka mtu katika hali mbaya na

umma.

Abdul, mfanyakazi wa hoteli kutoka

Ras Nungwi Kaskazini mwa Mkoa wa

Unguja ana mawazo kwamba umma

unapaswa kuelimishwa kutumia

sehemu kubwa ya rasilimali zake

kugharimia sekta ya elimu.

Lakini juu ya kwa nini upendeleo

uko zaidi kwenye arusi kuliko kwenye

elimu, Bw. Khamis anasema ni kwa

sababu arusi inaunganisha familia mbili

ambazo zinashindana, kila mmoja

ikitaka kuivutia nyingine.

Kila mtu kutoka upande wa familia

ya bwana arusi au bibi arusi anahisi

kwamba kuna haja ya kusherehekea

ambapo suala la elimu linahesabiwa

kuwa ndani ya familia moja yenyewe.

Anasema kuwa hakuna faida ya

moja kwa moja ya vitu kwa ndugu wa

mbali au marafiki wakati wanapotoa

mchango kwa ajili ya elimu ya mtoto

ambapo anasema unapochanga kwa

ajili ya arusi karibu unalazimika

kuhudhuria.

Anasema hii inaamaanisha kwamba

kila upande wa wenzi hawa unahisi

unawajibika kuchangia arusi kutokana

na woga tu kwamba iwapo hawatafanya

hivyo, upande mwingine utawafikiria

vibaya.

"Elimu inachukuliwa kuwa

shughuli ya mbali ya ukoo au shughuli

miongoni mwa watu wa familia

ambapo arusi inahusisha kundi kubwa

zaidi ambalo linajumuisha familia za

bwana arusi na bibi arusi zinazotoa

michango ziathirike," anasema.

Farashuu Ali Ame anasema kwamba

michango ya sherehe za arusi inatokana

na desturi ya muda mrefu ya kuamini

kwamba ndoa haiwi tu kati ya wenzi

bali ni muungano wa familia za bibi

arusi na bwana arusi.

Anasema

kwamba

kinachosherehekewa pale si ndoa ya

wenzi hao tu bali muungano wa hizo

familia mbili tofauti, ambao

unahalalisha sherehe kubwa zaidi.

Farashuu anadhani kwamba wakati

ambapo kuna haja kwa wazazi kupanga

ukusanyaji huo wa fedha uwawezesha

watoto wao kuhudhuria shule, hata

hivyo sherehe za arusi pia zidumishwe.

Khamisi Ali Shamte, mkazi wa

Kidongo Chekundu, anadhani

kwamba watu wanahisi kuwajibika

kuchangia sherehe za arusi kwa sababu

tu ya manufaa wanayoyatarajia ya

kushiriki katika hali ya usawa kwenye

sherehe yenyewe.

Anasema msukumo mkuu si

kusaidia bali kuwa sehemu ya watu

muhimu kabisa ambao wangependa

kusherehekea arusi.

JAMII NA WATOTO WALIO KATIKA HALI NGUMU

3

Watumishi

wastaafu

wawajali watoto

wa mitaani

NA JOSEPH KITHAMA

Ni jambo la kawaida kwa wastaafu wa serikali kutumia muda wao uliosalia wakihudumia biashara binafsi ili waweze kuishi kulingana na mapato, lakini watatu wao, wakiwa TemekeMtoni, Dar es salaam wana wito tofauti.

Wastaafu hao watatu wanautumia muda uliosalia kutoa elimu kwa watoto wa mitaani katika jiji na hivyo, kulilea wazo lao katika upendo mkubwa wa kuwafanya watoto wa mitaani waende shule, bila ya rasilimali zao wenyewe, hata kidogo na juu ya yote hawakuwa na jengo lolote lile la kuiendeshea shule yao.

"Mwaka 1968 tulisajili shule, kwa misingi ya hali ya utegemezi wa wafadhili ikiwa inalengwa kutoa elimu ya bure kwa watoto wa mitaani, hususan yatima, walioacha shule ya misingi na yatima wanaolazimika kuacha masomo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulipa ada ya shule pamoja na gharama nyinginezo," Mkurugenzi Mtendaji wa Dhamana ya Matunzo na Maendeleo ya Watoto wa Mitaani (SCCADET), Bw. Peter Nnaly

(69), lakini mstaafu, alisema.

Bw. Nnally, pamoja na Bw.Bernard

Makoja, mwalimu wa zamani ambaye

alijiunga katika siasa; na Mwalimu

Mkuu wa shule hiyo, Bi. Perpetua Nali,

hivi leo ni urithi wa kundi la

wafanyakazi wa serikali wastaafu

ambao wameshinda vishawishi vya asili

vya kushughulikia biashara zao

wenyewe ili kufuatilia kile

wanachokiona kuwa ni kusudi lenye

thamani.

"Wakati wa usiku tulianza kwa

kufuatilia sehemu za wazi ambazo

watoto wa mitaani walizitembelea

mara kwa mara, hususan wale

waliokuwa wakiuza vitu kama vile

sigara, karanga za kukaanga na maji ya

kunywa ili kuwashawishi wajiunge na

hii shule ya bure," Mkurugenzi

Mtendaji

wa

SCCADET

anakumbukia.

Kama mpango wa kuwavutia kwao,

wafanyakazi hao wa zamani wa serikali

wanalazimika kuwashawishi watoto wa

mitaani kwamba hawatapoteza biashara

ndogondogo ambazo zinawahakikishia

vipato vya kila siku kununulia walau

vitu vya msingi.

Mkutano wa Maaskofu wa Tanzania

Bw. Bernard Makoja (mwansiasa mstaafu) akimfundisha mtoto wa shule ya msingi

(TEC) uliipatia shule hiyo jengo la zamani huko Temeke Mtoni, ambalo lilikuwa likitumika kama baa ya bia. Kundi la mwanzo la wanafunzi halikuwa na madawati ya kukalia; badala yake walilazimika kusoma wakiwa wamekaa chini sakafuni.

Miaka miwili baadaye shule hiyo ilinyang'anywa jengo, jambo lililomshawishi Bw. Nnali awasiliane na ndugu zake ili watoe jengo dogo ambalo lilikuwa katika ushoroba wa mtaa wa vibandavibanda, ambavyo vilionekana kama vibanda vya kuku.

Ni Reverend Father John wa Benedictine Order ambaye aliwaunganisha na ufadhili wa Kijerumani kuhusiana na shule hiyo ambayo ilikuwa haifahamiki. Ikitumia fedha kutoka kwa mfadhili huyo, usimamizi uliibadili nyumba hiyo iliyoonekana kama banda la kuku

kuwa madarasa madogomadogo.

Hatimaye, juhudi za shule ya watoto

wa mitaani zilitambuliwa na Mfuko wa

Okoa Watoto Tanzania, ambao ulitoa

msaada wa vitu na wa kifedha kuisaidia

shule, ikiwa ni pamoja na posho ya

walimu wa kujitolea.

Mwaka 2002 juhudi za wachangiaji

wote ziliwezesha shule hiyo kuwa

miongoni mwa shule kumi za msingi

za kwanza zilizofanya vizuri katika

mitihani ya kitaifa ya Darasa la IV.

Hata hivyo, hiyo shule imeharibika

vibaya kufuatia kufungwa kwa Mfuko

wa Okoa Watoto. Watoto watatu tu

ndio waliofanikiwa kufanya mtihani

wa darala la VII mwaka 2003 kwa vile

watoto wengi walilazimika kuacha

masomo kutokana na matatizo ya

shuleni.

Shule haina maji ya bomba; milo ya

watoto

inategemea

fedha

zinazokusanywa na mwalimu mkuu kutoka kwa wanachama wenza wa Chama cha Wanawake Wakristo (WAWATA) na pamoja na waumini wengineo wa mitaani.

Dawati lililowekwa nje ya darasa linatumika kama mapokezi na meza ya chakula kwa jili ya wafanyakzi waliosalia, ambao wanatokana na wastaafu. Shule hiyo haijawahi kuwa na maji ya bomba, badala yake wanategemea maji ya mvua yanayochirizika kutoka kwenye mabati.

Hivi sasa, katika hali hiyo ya kusikitisha, shule hiyo ya watoto wa mitaani ina nafasi kumi za walimu zilizo wazi ambazo zinaweza kuendelea kuwa wazi siku zote kwa kuwa mfuko wa shule hauwezi kumudu kumlipia kila mwalimu mshahara wa Tsh. 50,000.

Watoto yatima wa `Malaika'

Onesphory, miongoni wa wajumbe wa kamati ya watoto yatima

Mtoto katika Kamati ya Yatima

Onesphory Gabriel ana umri wa miaka 13, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bugando.Yeye ni mjumbe wa Kamati ya MVC ya Bugando `A', akiwa Katibu wa Kamati hiyo. Onesphory anaifurahia kazi yake mpya, amepania kufanyakazi kwa bidii kama mwakilishi wa watoto wa Kata ya Bugando `A'.

Onesphory amefiwa na baba yake mwaka 1996, lakini mama yake anayefanyakazi kama Katibu Muhtasi katika Kampuni binafsi anamlea yeye na ndugu zake watatu; kaka yake mwenye umri wa miaka 16, dada yake pacha na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 10. Wote wanaishi pamoja kama familia.

Onesphory amechaguliwa katika Kamati ya MVC wakati wa mkutano wa Hadhara wa Kata wakati mchakato wa uainishaji wa MVC ulipotambulishwa katika jamii.

Onesphory na msichana mmoja walichaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Watoto Walio Hatarini Kabisa ya Kata ya Bugando `A', wakiwakilisha sauti za yatima na watoto wengine walio hatarini kabisa.

Uteuzi wa Onesphory na mwenzake ulifanywa na Mwenyekiti wa Kata, na watoto waliohudhuria mkutano huo waliombwa maoni yao, kuwa ama waunge mkono au wakatae uteuzi wao. Watoto hao waliridhia kuwa wawe wawakilishi wao katika Kamati ya MVC.

Baadaye alichaguliwa kuwa Katibu wa Kamati. Onesphory anachukulia jukumu hilo la jamii kwa dhati kabisa. Mwishoni mwa juma hutembelea kitongoji ili kubadilishana mawazo na watoto, na kujua hali zao. Yeye ndiye aliyetupeleka kwa Hassan na Samson, baada ya kujua mateso wayapatayo nyakati za ziara zake.

NA GODFREY KALAGHO,

DAR ES SALAAM

Mfuko wa Yatima wa Malaika ndilo jina ambalo Bibi Najma Manji alilichagua kwa ajili ya makazi ili kuamsha welewa wa umma ili jamii iweze kutambua umuhimu wa kuwaokoa na kuwalinda watoto wengi wanaoishi katika mazingira ya hatari. Neno Malaika linawafananisha watoto na Malaika wa Mungu.

Yeye ni mwangalizi wa mfuko; kituo ambacho hivi sasa kinawatunza watoto 15 walio chini ya umri wa miaka 12. Mwanzoni ilikuwa nyumba ya vyumba vinne vya kulala kwa ajili yake na familia yake.

Bibi Manji alianza kuwatunza yatima wakati alipoolewa. Hisia zake kali za kuwalea yatima zilioana na zile za mumewe, ambaye mwenyewe alikua akiwa yatima.

"Tulikuwa tukiishi na yatima humuhumu, kwenye nyumba yetu. Kadiri idadi yao ilivyoongezeka ndivyo tulivyokabiliwa na upungufu wa rasiliamli, lakini ilikuwa vigumu kupata msaada kutoka jamii ya ndani na au Asasi zisizo za kiserikali. Hili likatuchochea kujitolea nyumba yetu na kuigeuza kuwa kituo cha yatima", anasema.

Kati yao hao yatima 15, wawili ni yatima wa kijamii, ambao hivi sasa wanahudhuria shule ya awali pamoja na watano wengine. Sita wako darasa la kwanza wakati mmoja yuko katika shule ya watoto wenye mtindio wa ubongo iliyoko Sinza Dar es Salaam. Mkubwa kuliko wote ana umri wa miaka 15 na hivi sasa anajifunza kushona cherahani kwenye shule ya ufundi stadi.

Kwa vile ni makazi ya familia, eneo la nyumba ni dogo sana. Wavulana wanatumia vyumba viwili, ambapo wasichana wanatumia nyumba vilivyosalia. Pia, kuna wahudumu wanne ambao wanalala ukumbini.

Nilipoingia katika kila chumba, niliona magodoro matatu au manne yamelundikwa kwenye kitanda kimoja na baadaye nilielewa kwamba yalikuwa ya wahudumu wa kike. Kila asubuhi wanapaswa waondoe mikeka yao ya kulalia na matandiko ukumbini ili sehemu hiyo iweze kutumika kama mapokezi.

"Sehemu hii ni ndogo sana, tunahitaji kuipanua, lakini hatuna fedha, "Bibi Manji alisema, akiongeza kwamba wilaya ya Kinondoni ina yatima wengi na kwamba wale walioko Malaika wana bahati kwa kuwa kituo hicho hakiwezi kuchukua zaidi.

"Idara ya Ustawi wa Jamii bado inawashauri watoto waje hapo, lakini hatuwachukui kwa kutokana na ukosefu wa nafasi," alisema.

Mchana, watoto walirejea toka shule na ulikuwa wakati wa chakula cha mchana. Watoto wengine wa mtaani walio chini ya umri wa miaka kumi, ambao wanakosa vituo vya malezi, walikuwa wamekwishafika, wakisubiri chakula.

Katika kituo hiki watoto wanaishi kama dada na kaka wa familia moja. Wanahusiana vizuri sana na watoto wa wengine ambao hawakupata nafasi, wanakula, wanacheza na kuimba pamoja.

Hata hivyo, baada ya kula, yatima wa Malaika wana ratiba ya kudumu ya shughuli nyingine na wanapaswa waondoke kwenda sehemu nyingine.

Maria Athuman, mwenye umri wa miaka 8, hana shaka kwamba Bibi Manji ndiye mama yake. Nilipomuuliza kuhusu wazazi wake, alinijibu: "Maka yangu huyu hapa," alisema akimwelezea Bibi Manji.

Ingawa kituo hicho ni safi sana, lakini Bibi Manji anawasiwasi juu ya mambo matatu. Kwanza, ni mateso ya watoto ambao bado hawajapata nafasi katika nyumba ya yatima na wanazurura mitaani wakiokoteza chakula. Anasema serikali imewapa ekari 50 huko wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, lakini hawana pesa kuweza kuendeleza sehemu hiyo.

Pili, kituoni kuna uhaba wa maji. Ili kulijaza tanki, hawana budi kuteka maji kutoka mbali. "Kama mtoto akiugua na hakuna maji, anaweza akawaambukiza wengine kwa urahisi kabisa," anasema.

Tanki la maji lililopo lililotolewa na Shirika la Kikristo.

Tatu, Ingawa watoto hupata huduma ya tiba bila malipo kutoka hospitali za serikali, lakini gharama za tiba ni tatizo iwapo dawa zilizoandikwa hazipatikani kwa urahisi. "Inakuwa gharama kwa sababu unalazimika kwenda kwenye maduka ya dawa binafsi ambako dawa ni ghali," anasema.

Habibu Henry, mwenye umri wa miaka 12, ambaye amepooza upande mmoja, anaishi katika kituo hiki. Kwa vile hawezi kutembea bila msaada, kila mara husindikizwa shule. Aliokolewa na Chama cha Wawindaji katika Mkoa wa Iringa. Chama hicho ndicho kilichomleta Dar es salaam kwa ajili ya matibabu.

Alipoletwa kwenye Idara ya Ustawi wa Jamii, Dar es salaam, ikagunduliwa ya kwamba mtoto huyo pia alikuwa na matatizo ya akili. Hili likaifanya menejimenti ya Malaika kumtafutia shule maalumu ? kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya ulemavu. Ilikuwa hatua isiyofaa.

Bw. Chelestino Msimbwa, Mwalimu Mkuu wa Shule Maalumu ya Sinza, ambako Habibu anasoma, ambaye mara moja aliwahi kumsindikiza mtoto huyo hospitali, alisema kwamba madaktari waligundua kwamba

Habibu anaugua ugonjwa wa "macho

kufifia" (optical atrophe). Hii ina maana ya

kwamba neva ya jicho imeathirika, na

kusababisha kuunganishwa kwa ujumbe

kutoka kwenye jicho kwenda kwenye

ubongo kwa ajili ya fasili. Alisema

anaendela vema katika masomo yake.

Bibi Betty Shija, Mwalimu mkuu wa

shule hiyo alisema kwamba Habibu haoni

vizuri "Anapata kivuli, lakini hawezi

kusoma vizuri." Idara ya Ustawi wa Jamii

walituhumu tatizo hilohilo, wakiamini

kwamba linatokana na matatizo yake ya

awali; lakini amedhihirisha kuwa wa

kawaida kabisa.

Kutokana na matatizo ya kuona

anakwepa kukutanisha nyuso na ni

mchangamfu na kama akiulizwa hupenda

kuongea juu ya mustakabali wake. Hutoa

maelezo mazuri juu ya uzoefu wake

uliopita.

"Nilizaliwa Mabalali katika mkoa wa

Iringa, nilikuwa mtoto wa kawaida Mama

yangu ni Sikamanga na baba yangu Henry

Ming'engeji. Baadaye nikatambua kwamba

siwezi kutumia mkono na mguu wangu wa

kulia. Macho yangu pia yalikuwa yanawasha

na nilipata maumivu makali. Baadaye

macho yangu yakawa dhaifu na karibu

sikuweza kudhibiti matendo yake," alisema.

Anasema madaktari wa CCBRT Dar es

Salaam

walimwambia

kwamba

wasingempasua kwa sababu ingehatarisha

maisha yake na huenda angekuwa kipofu

kabisa.

Habibu alisema kwamba aliwapoteza

wazazi wake wote wawili na akawa anaishi

na dada yake, Sipendeki. Ingawa yu salama

katika makazi ya Mfuko wa Yatima wa

Malaika, ana wasiwasi juu ya mdogo wake

wa kiume Mateso, alisema hana uhakika

kuhusu usalama wake.

"Nikikua, napenda kuwa mwalimu,

nijenge nyumba yangu mwenyewe na

kuendesha gari langu mwenyewe; anasema.

"Lakini kamwe sitaondoka Malaika,"

anasisitiza.

Anaamini kwake Malaika ni kwao, kama

ilivyo Iringa. Ari na matumaini yake

vinategemea watu wanaowalea yatima wa

Malaika.

Bibi Manji anauendesha mfuko huo

kwa msaada wa wanafunzi wake wawili wa

zamani katika shule ya msingi, ambao

aliwafundisha 1978. Wanafunzi hao ni

Hadija Membungu na Bahati Godfrey.

Majirani huwasaidia kwa ngano, sukari na

chumvi, kila wanapoombwa wasaidie.

Wamiliki wa maduka wanawakatalia

kuwakopesha

bidhaa

kila

wanapojitambulisha kama wahudumu

kutoka Mfuko wa Malaika.

4

Hali ya watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu

Idadi ya watoto yatima hapa nchini ni zaidi ya milioni mbili. Yatima wanakabiliwa na mahitaji muhimu ambayo wamekuwa hawayapati kwa kiwango kinachotakiwa. Watoto wengi zaidi wamekuwa wana beba majukumu mazito yanayoshinda

umri wao: Kama vile kuwa kiongozi wa familia, kutunza wazazi wagonjwa na kufanya kazi kwa muda mrefu ili kujipatia riziki.

Mtoto anayeisha na mmoja au wazazi wake wote wakiwa wagonjwa, hushindwa kwenda shule, kwa

kuwa lazima atafute pesa kwa kufanya kazi za ziada ikiwa ni pamoja na kulima.

Ingawa mtoto huyo si yatima, lakini atakosa haki zake nyingi za msingi na atajikuta katika hatari ya kunyonywa na kudhalilishwa.

Habari zote na UNICEF Tanzania

Kina bibi ndiyo walezi wakubwa wa yatima Tanzania

Eliza Kulola, ana umri wa miaka 68, na ni mjane. Akiwa amekaa katika mkeka nje ya kibanda kilichoezekwa nyasi na kuku wakila, Eliza anazungumzia mzigo wa kulea wajukuu watano akiwa peke yake.

Wajukuu wa Eliza wana umri wa

miaka 16,15,13,7 na 4. Anaishi nao wote

katika kijiji cha Nyagusa, tangu wafiwe na

mama zao. Anaonekana amechoka na

kukosa matumaini wakati akizungumzia

maisha yake na familia aliyonayo hivi sasa.

Kwa sasa wasiwasi wake ni hatima ya

watoto," Kusema kweli, sifikirii namna ya

kuwalisha wajukuu zangu, kwa sababu

kutoka shamba langu dogo na misaada ya

jirani tunaishi. Wasiwasi wangu zaidi ni

majaaliwa yao baada ya mimi kufariki,

mimi ni mzee na hushambuliwa na

malaria mara kwa mara, Sijui!," alisema

Eliza huku akiwa amekaa mkekani akiwa

na kitukuu chake cha umri wa miezi 8 Eliza Kulola (miaka68 ) akiwa na wajukuu (kutoka kushoto) Neema

magotini.

(miaka 13), akiwa amapakata Moses (miezi 8), Noel (miaka4) na

Kwa miaka 7 iliyopita Eliza amekuwa Zacharia (miaka7)

akiwauguza mabinti zake watatu mmoja baada ya mwingine, mpaka walipokufa na kuwaacha watoto 5. Mpaka

sasa Eliza anategemea zaidi kilimo cha kawaida kujipatia riziki. Analima mhogo na mtama karibu ya nyumba yake,

kiasi cha kujipatia chakula, aidha anauza kuni kufidia mahitaji ya kaya. Hajawahi kusoma na mpaka sasa hawezi

kusoma wala kuandika.

Miongoni mwa wajukuu zake ?Emma 7, Jennifer 9 na Neema 13, ndio wapenzi wake, kwa sababu wanasaidia

kazi za nyumbani. Wasichana hao wanakata kuni kwa ajili ya kupikia na kuuza, kuteka maji, kumtunza mtoto wa

miaka 4. Bila shaka, kazi zote za nyumabni zinawaangalia wao. Ingawa wanasoma, hawana muda wa kujisomea

nyumbani au kufurahia utoto wao.

Neema, 13, anajua machache kuhusu baba yao. anajua kuwa ni askari. Hajafika kuwaangalia, tangu mama yao

afariki dunia miaka 5 iliyopita. Neema anapenda shule, na anahakikisha kuwa anaweza kununua madaftari yake ya

shule kwa kuuza kuni. Bei ya mzigo mmoja wa kuni ni sh. 200 (sawa na robo dola ? senti 20).

Bibi Eliza anaonekana amechoka, ndio anapata nafuu ya malaria, na ana wasiwasi kuwa mbu watawang'ata

wajukuu wake. Wanalala pamoja katika chumba kimoja, hawatumii chandarua kwa sababu hawana uwezo wa

kununua.

Watoto kama Watunzaji Wazazi Wagonjwa

Katika umri mdogo sana,Veronika Simon tayari ni mtu mwenye majukumu ya familia na kumtunza mama yake mgonjwa. Msichana huyo ana umri wa miaka 13 na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nundu. Veronika anaishi na

mama yake Lucia Ganzia aliyefikisha umri wa miaka 50, ingawa

anaonekana kama ajuza wa miaka 70. Hapana shaka, UKIMWI

umedhoofisha mfumo wake wa kinga na kukondesha mwili wake.

Anazungumza na kutembea kwa taabu sana, na akipata nguvu ya

kusema utaona hisia ya maumivu usoni mwake.

Lucia anaishi na mjukuu wake Yohana Simon mwenye umri wa

miaka 11. Yohana anasoma pamoja na Veronica. Lucia anategemea

sana ukoo wake mpana na wasamaria wema kuwalisha na kuwavalisha

watoto wake, na kadiri anavyozidi kuugua na kudhoofika, msaada wa

familia unazidi kupungua na anategemea zaidi Kituo cha UKIMWI

cha jamii.

Hata siku tulipowatembelea, Veronica alikuwa amemsindikiza

mama yake katika Kituo cha Mapumziko cha UKIMWI cha

MWAOMI, kuchukua dawa na chakula. Kituo hicho kinamilikiwa na

Kanisa la Anglikana, kikitoa msaada wa wastani kwa watu

wanaoathiriwa na VVU/UKIMWI.

Veronica Simon anamuuguza mama yake

Lucia anajiona mjane, kwa sababu tangu mwaka 1997 hajawasiliana aliye taabani

na mume wake, baba wa watoto wake.

Lucia ameonekana na virusi vya UKIMWI mwaka 1997, na ana uhakika kuwa ameambukizwa na mume wake,

aliyekuwa akiumwa mara kwa mara lakini alikataa kukubali au kwenda kupimwa. Alianza kuumwa mwaka 1998,

aliumwa kiasi cha majirani kumpeleka hospitali na kulazwa katika wadi ya wagonjwa wa TB. Mtoto wake wa kiume

ambaye wakati ule alikuwa na umri wa miaka 11 ndiye aliyekuwa mlezi mkuu; kupika na kupeleka chakula

hospitali.

Kwa miaka yote, Lucia amekuwa akilazwa na kutolewa hospitali kwa maradhi mbalimbali na maambukizo

nyemelezi, na Veronica ndiye pekee anayehudumia mahitaji yake. Ana wasiwasi kwamba mtoto wake wa kiume

mara nyingi hayupo nyumbani kwa sababu amechoka kumhudumia.

Veronica yuko darasa la 5 lakini mahudhurio yake yamekuwa mabaya; wakati mwingine haendi shule kwa

majuma kadhaa, kwa vile anakaa nyumbani kumhudumia mama yake mgonjwa. Familia inamtegemea Veronica

kutafuta fedha. Msichana huyo anapika maandazi anayouza duka la jirani. Wakati mwingine Lucia anapojisikia

ahueni, anamsaidia binti yake kukanda maandazi.

Kadiri afya ya Lucia inavyozidi kuwa mbaya, hakuna hata mmoja katika ukoo mpana aliyejitokeza kuzungumza

naye kuhusu majaaliwa ya watoto wawili. Kwa Lucia ina maana kuwa hakuna hata mmoja anayetaka kuchukua

jukumu la kulea watoto, na hili linamvunja moyo, kwa kufikiri wataishije baada ya yeye kufariki dunia!

Familia zabebeshwa mzigo mzito

Kata ya Bugando Mission, Mwanza. Samson ana umri wa miaka 8, Hassan 10 na Rahel Khalfan 14 na wote ni yatima, waliofiwa na wazazi wao miaka mingi iliyopita. Rahel na Hasaan angalau wanakumbukumbu za baba yao, kuwa mkulima aliyemiliki shamba kubwa. Hawakumbuki kijiji walichokuwa wakiishi, ila tu ilikuwa Mkoa wa

Uporaji wa urithi wa watoto

Juma Joseph, umri wa miaka 15, alikuwa darasa la 5 katika Shule ya Msingi Bungarika kabla ya kuacha shule. Hivi sasa anazurura, akipitisha muda wake vijiweni.

Juma ameacha shule kwa sababu alirudishwa nyumbani na waalimu kwa kukosa sare za shule. Alipomwambia

mjomba wake, alikataa kumnunulia sare na kumlazimisha arudi shule akawaambie walimu kuwa "hakuna mtu wa

kununua sare" Mtoto alikataa kurudi kwa kuogopa kuaibishwa na hivyo kuamua kubaki nyumbani.

Mjomba wao aliamua kuwachukua baada ya baba yao kufariki, amekuwa akimtesa Juma na mdogo wake.

Mara nyingi juma anafokewa na kujenga chuki kati yake na mjomba wake. Amekuwa akimwambia Juma kuwa

hawezi kuendelea kumlisha yeye na mdogo wake Emmanuel mwenye umri wa miaka 12.

Juma na Emmanuel ni yatima, wamefiwa na wazazi wao wote tangu mwaka 1999 na 2000; Baba yao alitangulia

kufariki dunia, halafu akafuatia mama yao. Hawajui kilichowaua wazazi wao, lakini wanakumbuka tu kwamba wote

walikuwa nyondenyonde kila siku, na walikuwa wakienda hospitali mara kwa mara.Wala hakuna hata mtu mmoja

aliyewaambia kilichokuwa kikiwasumbua.

Baba yake Juma ana nyumba walioozoea kuishi kama familia. Baada ya kifo cha mama yao, Juma na Emmanuel

walihamishiwa kijijini kuishi na shangazi zao. Maisha yalikuwa magumu kijijini kwa sababu shule ilikuwa mbali

na watoto walikuwa wamechanganyikiwa. "Kaka yao mkubwa aliamua kuwarudisha mjini, na kujiunga tena na

shule yao ya zamani.

Watoto walipata pigo la pili wakati kaka yao mkubwa alipougua na baada ya kwenda hospitali akapimwa na

kugunduliwa ana T.B. Alidhoofika haraka na kufariki mwaka 2004.

Walihamishiwa kwa ndugu mwingine, mjomba, wanakoishi hivi sasa. Mjomba wao anayewalea ndiye pia

mdhamini wa nyumba yao ya familia. Ameikodisha nyumba hiyo, anakusanya kodi kila mwezi na kutumia fedha

hizo kwa matumizi yake ya binafsi.

Amewaambia watoto hao kuwa fedha ya pango anayokusanya ndiyo wanayotumia katika familia kwa chakula

na mahitaji mengine

madogo madogo.

Juma

na

Emmanuel wanajua

wazi

kwamba

anachofanya mjomba

wao si haki, lakini

ndugu zao wote

wamenyamaza.

Wanajaribu kuomba

msaada kutoka kwa

viongozi wa kijiji,

lakini mlolongo ni

mrefu na wa polepole

mno! Juma bado

haendi shule na

haielekei

kama

atarudia shule yake

hivi karibuni!

Juma (miaka 15) na Emmanuel (mika 12) wameporwa nyumba yao na mjomba

Kigoma. Rahel

anakumbuka kuwa

ilikuwa upande gari

la moshi ili ufike

kijijini kwao.

Watoto hao hivi

sasa wanaishi na

Ashura Chishako,

ambaye ni dada wa

marehemu mama

yao. Ashura ni mjane

Mama mmoja anayeishi Wilayani Makete akiwa na wanae pamoja na watoto yatima wa ndugu zake

baada ya mume wake kumtelekeza na watoto 8. Ashura

hajasoma, yeye ni mchuuzi wa ndizi na anajipatia Tsh. 500 kwa siku (sawa na nusu dola) na kulisha familia ya watu

12.

Watoto wamechanganyikiwa, wamevaa matambara (nguo mbovu), wana njaa na Hassan alikuwa analia.

Wavulana wawili wanasoma shule ya msingi Bugarika, lakini msichana anabaki nyumbani kusaidia kazi zisizo na

kikomo na kuuza ndizi. Samson ni mzungumzaji sana, na anaeleza haraka maisha yao na shangazi yao Ashura mjini

Mwanza.

Sentensi ya kwanza ya Samson ni kwamba wanakula mara moja kwa siku wakati mwingine hata huo mlo mmoja

unakosekana. Kwa kuwa ilikuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani msimu wa waislamu kufunga saumu Samson

husema kuwa "Ni afadhali tufunge saumu, kwa sababu hatuli chochote mchana."

Samson na kaka yake hawana chumba katika nyumba ya familia, kwa sababu kitanda kimoja analalia shangazi

yao na baadhi ya watoto wadogo na wasichana wakubwa wanalala ukumbini. Wavulana wanalala stoo, kunakolala

kuku na mabata. Wanalala chini kwa kujifunika magunia ya zamani. Mahali hapo ni pabaya sana! Samsoni amesema

kuwa usiku mifugo inawasumbua kwa kuwanyia usoni, mikononi na miguuni.

Shangazi yao huwatukana na kuwapiga kiasi cha kuwaudhi. Ili kuongezea mapato ya familia, wavulana na dada

yao lazima wafanyekazi sana. Wavulana wamejenga tabia ya kufanya kazi kila siku ya kuokota mkaa katika jaa la jiji

kwa matumizi ya nyumbani kila wanaporudi shule. Wakati mwingine wanapokosa mkaa wa kutosha, shangazi yao

huwapiga na kulala bila ya chakula.

Samson anaonekana kuwa mzigo na mtundu zaidi. Siku moja Ashura alimpa Samson Tsh. 200 akanunue nyanya,

lakini alinunua za Tsh. 100 tu na kutumia 100 nyingine kununulia maandazi. Shangazi alikasirika na kumpiga sana

mpaka majirani wakaingilia kati. Tukio hilo la unyanyasaji limeripotiwa Polisi, walimwomba shangazi ajaribu

kuwatendea ubinadamu watoto hao. Tabia ya Samson inamkasirisha sana Shangazi yake.

Ni dhahiri kwamba mzigo wa kuwa mkuu wa kaya kubwa kama hiyo ni mzito mno kwa mama mjane kama

Ashura. Mfumo wa ukoo mpana ulitumika kuwalea yatima kutoka ndugu zao unakuwa mzigo mzito!

Kwa maoni: Andika Kitengo cha Mawasiliano UNICEF Tanzania P.O. Box 4076 Dar es Salaam, Barua pepe: daressalaam@ Kwa habari zaidi soma:

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download