ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI ...

ATHARI ZA KIMOFOFONOLOJIA ZA KIOLUSUBA KATIKA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU KAMA LUGHA YA PILI

MEROLYNE ACHIENG OTIENDE

Tasnifu hii imewasilishwa kwa ajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Nairobi.

(2013)

UNGAMO

Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijatolewa kwa mahitaji ya Digrii katika chuo kingine.

________________________ (Mtahiniwa)

Merolyne Achieng Otiende

Tarehe: ______________

Tasnifu hii imetolewa kutahiniwa kwa idhini yetu kama wasimamizi wa kazi hii.

_______________________________ Dkt. Iribe Mwangi

Tarehe: ___________________

________________________________ Bi. Mary Ndungu

(Wasimamizi)

Tarehe: ___________________

ii

TABARUKU Naitabaruku kazi hii kwa mume wangu mpendwa Paul Rabala Oloo kwa imani aliyo nayo katika uwezo wangu. Pia kwa vito vya maisha yangu Wren, Avyn na Valene kwa

kunihimiza kutia bidii.

iii

SHUKRANI Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuyakamilisha masomo yangu ya uzamili na pia kuikamilisha kazi hii. Hakika kazi kama hii haiwezi kukamilika bila msaada wa wengine. Ningependa kuzitoa shukrani zangu za dhati kwa wote waliochangia kwa njia moja au nyingine katika ufanisi wa utafiti huu. Kwanza kabisa nawashukuru wasimamizi wangu Dkt. Iribe Mwangi na Bi. Mary Ndungu ambao waliniongoza kutoka mwanzo hadi nilipoikamilisha kazi hii. Daima nitawashukururu na kuwatakieni kheri na baraka zake Mterehemezi. Pili, nawashukuru walimu wangu wote. Aidha namshukuru Prof. Okoth Okombo kwa mawaidha aliyonipa mwanzoni mwa utafiti huu. Vile vile nawashukuru walimu wa shule za msingi za Uozi, Wakinga na Gethsemane kwa kuniruhusu kutangamana na wanafunzi wao na kupata baadhi ya data iliyofanikisha utafiti huu. Hali kadhalika nawashukuru watangazaji wa kituo cha redio cha Ekialo Kiona wakiongozwa na Bonfas Msaswa kwa maelezo ya kina waliyonipa kuhusu masuala mbalimbali ya Kiolusuba. Sitamhini shukrani zangu mzee Fabian Ouma aliyenieleza mambo kadhaa kuhusu data ya utafiti huu. Siwezi kuwasahau wanafunzi wenzangu tulioabiri nao chombo hiki kwa kunitia moyo kila mwendo ulipoonekana kuwa mgumu. Hao ni pamoja na Lily Chebet, Lydia Moraa,Grace Kanyua, Juliet Okeyo na Francis Onyonka. Shukrani za kipekee kwa mume wangu Paul Rabala Oloo ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kunihimiza kulenga juu masomoni na pia kunifadhili kwa hali na mali kuhakikisha nimefaulu. Pia, sitawasahau wanangu Wren, Avyn na Valene kwa subira waliyokuwa nayo na kuvumilia upweke wa `mama asiyekuwepo' kila nilipowaacha na kwenda maktabani. Ninajua kunao wengi waliochangia ambao sijawataja kwa ukosefu wa muda . Kwenu nyote nasema. Ahsante.

iv

ISHARA NA VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA

[ ] Mabano ya fonimu

/ / Mabano ya fonetiki

{ } Mabano ya mofu

+

Mpaka wa mofu

$

Mpaka wa silabi

#

Mpaka wa neno

Inabadilika na kuwa

I Irabu

L1 Lugha ya kwanza L2 Lugha ya pili FZ Fonolojia Zalishi

NFZA Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia

Kip Kipasuo

Kons Konsonanti

Naz Nazali

Kiz-kikw Kizuiwa kikwamizwa

Mh Mhariri

Mid-meno Midomo na meno

v

................
................

In order to avoid copyright disputes, this page is only a partial summary.

Google Online Preview   Download